• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Vijana 664 Mkoani Simiyu Kunufaika na Ajira za Muda Msimu Mpya wa Kilimo

Posted on: November 25th, 2020

Takribani vijana 664 mkoani Simiyu wanatarajia kunufaika  na ajira za muda katika msimu huu  ,baada ya kupata mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu kwa ajili ya kukabiliana na wadudu wasumbufu wa zao la Pamba.

Hayo yamebainishwa jana Novemba 24, 2020 wakati wa kufunga mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu kwa wapuliziaji sumu katika zao la pamba yaliyotolewa na Gatsby Africa kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa Viuatilifu (TPRI) katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu ambayo yalihitimishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga.

Vijana hao wamebainisha mafunzo waliyoyapata pamoja na kuwasaidia kupata ajira yatawawezesha kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba kwa kuwa wamefahamu matumizi sahihi ya viuatilifu ilinganishwa na awali walipokuwa wakifanya kazi hiyo kienyeji.

“Tulikuwa tunafanya kienyeji lakini kwa sasa tumepata ujuzi mfano tumejifunza ni dawa ipi inatumika kuua aina gani ya wadudu kwa wakati gani; lakini pia tumejifunza ni kwa namna gani tunaweza kutumia viuatilifu pasipo kuathiri mazingira yetu,” alisema Samwel Salum mpuliziaji viuatilifu vya zao la pamba Meatu.

“Mafunzo haya kwangu yana umuhimu mkubwa sana maana nitakuwa nikipulizia viuatilifu kwenye mashamba ya wakulima napata hela, lakini pia nitatumia mbinu nilizojifunza kupulizia kwenye mashamba yangu na nitaongeza uzalishaji,” alisema Mayunga Mlyaza mpuliziaji viuatilifu vya zao la pamba Meatu.

Afisa Kilimo wa Kata ya Sakasaka Wilayani Meatu, Sylvester Mholi amesema mafunzo hayo yamewaongezea uwezo wa kujiamini katika kutambua viuatilifu ambavyo vinasambazwa na wasambazaji kwa kuzingatia sheria na miongozo mbalimbali inayohitajika.

Mwakilishi wa Gatsby Africa shirika lililoshirikiana na Mkoa kuandaa mkakati wa mapinduzi kilimo cha pamba (2019-2024) katika mafunzo hayo Bw.Michael  Kahindi amesema wakulima waliofikiwa na wapuliziaji hawa wa viuatilifu katika msimu uliopita wamefanikiwa kuongeza tija katika Uzalishaji wa pamba kutoka kilo 250 mpaka kufikia kilo 600 kwa hekali.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga amesisitiza uadilifu wakati wa utekelezaji zoezi la upuliziaji dawa katika mashamba ya wakulima “tusifanye udanganyifu kwa wakulima, ukimdanganya mteja wako kesho hatarudi tena kwako; sisi kama mkoa tunaona fahari kuwa tunao vijana 664 ambao tumewaongezea thamani kwenye kazi walizonazo.”

Mtafiti wa kudhibiti visumbufu vya mazao/mimea kutoka Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu nchini(TPRI), Bw. Ramadhan Kilewa amesema matarajio ya TPRI ni kuwa vijana hao wataenda kufanya kazi nzuri baada ya mafunzo hayo kwa kuwa awali baadhi yao walieleza kuwa walikuwa wakifanya kazi hiyo tofauti na maelekezo ya matumizi sahihi ya viuatilifu.

Kwa upande wake kaimu Katibu Tawala Msaidizi-Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji, Bibi. Kija Kayenze amesema “Lengo ni kuongeza tija hivyo tunatarajia tija itaongezeka sana kwa sababu wakulima wengi watakuwa wameshapata elimu sahihi ya matumizi ya viuatilifu.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa