• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Vifo vya Watoto Wachanga Vyapungua Simiyu

Posted on: September 25th, 2018

Vifo vya Watoto Wachanga mkoani Simiyu vimepungua kutokana na Serikali kutoa elimu ya uzazi na wazazi kuanza kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye semina ya Mkunga Okoa Maisha iliyofanyika mwishoni mwa wiki jana mjini Bariadi, Katibu wa Wakunga mkoani humo Daud Marwa alisema vifo vimepungua kutokana na jamii kuanza kujenga tabia ya kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya.                                        

Alisema kwa mkoa wa Simiyu mwaka 2016 walizaliwa watoto 47,193 lakini waliokufa walikuwa 655, mwaka 2017 walizaliwa watoto 38,442 na walikufa watoto 617 huku mwaka huu wamezaliwa watoto 37,098 na hadi Septemba wamefariki watoto 290.

“Vifo vya Watoto Wachanga mkoani Simiyu vimepungua kutoka 617 mwaka 2017 na kufikia 290 hadi mwezi septemba mwaka huu kutokana serikali kutoa elimu ya uzazi na wazazi kuanza kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya, hii ni jitihada kubwa sana kwani wakunga wamekuwa wakipatiwa mafunzo mara kwa mara, pia kuongezewa stadi za kumhudumia mama na mtoto mwenye uhitaji pindi anapozaliwa’’ alisema Marwa.

Aliongeza kuwa timu ya watumishi wa afya inaendelea kufanya ufuatiliaji na usimamizi ili kuhakikisha kila mama mjamzito anajifungua salama na mtoto mchanga anaendelea kuishi akiwa salama.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Mkunga Okoa Maisha Martha Rimoy alisema akinamama wajawazito wengi wao wanapoteza maisha kutokana na kutoka damu nyingi kabla ya kujifungua, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.

Alisema wanawake 556 kati ya vizazi hai 100,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na kutokwa damu wakati wa kujifungua na kifafa cha mimba, uzazi pingamizi, na uambukizo.

Aliongeza kuwa kutokana na takwimu hizo, hali ya vifo vya wakinamama na watoto wachanga bado ni mbaya sana hivyo serikali, wadau wa maendeleo na wananchi wanatakiwa kupiga vita vifo hivyo.

Aidha,  katibu huyo alisema baadhi ya wanawake mkoani Simiyu bado wanajifungulia majumbani kutokana na kuwepo kwa wakunga wa jadi na akabainisha kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wakina mama ili waache tabia hiyo badala yake wajifungulie katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuepuka vifo vinavyoweza kuzuilika.

 

‘’Tunaendelea kutoa elimu kwa wakunga wa jadi na wakinamama wajawazito ili wakipata matatizo ambayo yanazuilika waweze kuwahi vituo vya kutolea huduma za afya, kutoa mafunzo kwa watoa huduma na pia kuboresha sehemu za kutolea huduma’’ alisema Martha Rimoyi.

Naye Katibu Mkuu wa chama cha Wakunga nchini ambaye pia ni Mwalimu wa Wakunga chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi (MUHAS) Dkt. Sebalda Leshabari alisema kazi ya mkunga ni kumshauri mama mjamzito juu ya masuala ya uzazi hadi anapojifungua, lakini kazi ya muuguzi ni kuhudumia mgonjwa.

Alisema wakunga ni watu wenye taaluma ya ukunga na wenye stadi za kuhudumia mama mjamzito, wenye kugundua viashiria vya hatari kwa wajawazito na kutoa rufaa tofauti na wakunga wa jadi ambao hawana taaluma yoyote.

‘’Wakunga wa jadi hawana stadi na utaalamu pindi mama mjamzito anapokuwa na dalili za kushindwa kujifungua salama, hivyo tunawaomba wakinamama wajawazito wajenge tabia ya kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya ili kuzuiwa vifo visivyokuwa vya lazima’’ alisema Dkt. Leshabari.

Semina hiyo ya siku moja kwa waandishi wa Habari mkoa wa Simiyu ililenga kuwajengea uelewa na kufahamu juu ya mkunga, muuguzi na mkunga wa jadi kupitia mradi wa Mkunga Okoa Maisha unaolenga kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto wachanga.

MWISHO.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa