• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Upungufu wa Damu kwa Wanawake Wenye Umri wa Kuzaa Wapungua Simiyu

Posted on: November 12th, 2020

Changamoto ya upungufu wa damu kwa wanawake wenye umri wa kuzaa mkoani Simiyu imepungua kutoka asilimia 57 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 34 mwaka 2019 kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na viongozi, watendaji na wananchi, ikiwa ni pamoja na kulipa kipaumbele suala la lishe.

Hayo yamebainishwa na Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige wakati akiwasilisha taarifa katika kikao cha kamati ya lishe ya mkoa kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.

Magige amesema Elimu ya kujirudiarudia imewafanya wananchi wapate uelewa wa kutosha juu ya ulaji sahihi ambapo amesisitiza kuwa pamoja na elimu mkoa uliweka mkakati kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuongeza nguvu katika katika utoaji wa vidonge vya kuongeza damu kwa wasichana.

“Suala la lishe limepewa kipaumbele katika mkoa wetu na elimu inaendelea kutolewa katika vituo vya kutolea huduma za afya, ngazi ya jamii ambapo wanawake wanafundishwa kuandaa chakula kwa usahihi katika makundi yote matano ya vyakula,” alisema Dkt. Magige.

Katika hatua nyingine Magige amesema katika kukabiliana na udumavu mkoani Simiyu, Mkoa umejiwekea mikakati kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya namna ya kuandaa vyakula vya kuwalisha watoto walio vituo vya kutolea huduma za afya na ngazi ya jamii, elimu ya unyonyeshaji sahih,  elimu ya mabadiliko ya ulaji na kuhimiza wananchi kwenda kuapata matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Akizungumza na wajumbe wa kamati ya lishe ya mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bibi. Miriam Mmbaga ametoa rai kwa viongozi na watendaji kuendelea kutimiza wajibu wao na kila mmoja kutambua kuwa suala la lishe ni la muhimu huku akisisitiza ushirikiano ili kuwaokoa wananchi wa mkoa wa Simiyu kuondokana na athari zitokanazo na lishe duni.

Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bi. Happiness Kubona amesema Maafisa Lishe wataendelea kuwajengea uwezo wahudumu wa afyangazi ya jamii, ngazi ya vituo kuwatambua watoto wenye utapiamlo na kuwaingiza katika matibabu .

Ameongeza kuwa hamasa ya kujiunga na Mfuko Afya ya Jamii ulioboreshwa(ICHF) kwa wananchi itaendelea kutolewa ili waweze kupata huduma za matibabu na  hususani wanawake waweze kupata huduam ya vidonge vya kuongeza damu ili wasipungukiwa damu wakati wa ujauzito.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/11/upungufu-wa-damu-kwa-wanawake-wenye.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa