• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Ununuzi Mazao Mchanganyiko Kupitia AMCOS Utawakomboa Wakulima: DC Bariadi

Posted on: March 11th, 2020

Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema  mfumo wa ununuzi wa mazao mchanganyiko kupitia vyama vya msingi vya Ushirika ( AMCOS) utakaoanza kutekelezwa mwaka huu 2020 umelenga kuwakomboa wakulima na  kuwawezesha kupata soko la uhakika  lenye ushindani pamoja na kuwaondoa wanunuzi wanyonyaji.

Kiswaga ameyasema  hayo jana katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika shule ya sekondari Kusekwa Memorial mjini Bariadi mkoani Simiyu, lengo lilikuwa kujadiliana namna ya kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.  Hussein Bashe kupitia tangazo alilolitoa Februari 14, 2020 kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko,dengu ,mbaazi , na soya kupitia Vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS)  kwa mikoa yote inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.

Amesema wakulima wa mazao ya jamii ya mikunde pamoja na mbegu wamekuwa wakiuza kiholela pasipokuwa na mfumo rasmi hali iliyokuwa ikipelekea kuuza kwenye mizani ambayo haijahakikiwa huku wanunuzi wakijiamlia bei wanazozitaka.

"Serikali  imeamua kuja na mpango huo mzuri na lengo lake kubwa  ni kuwakomboa wakulima pamoja na kuwaondoa wanunuzi wanyonyaji kwani wamekuwa wakinunua mazao kwa wakulima kwa bei zao wenyewe jambo ambalo linapelekea kuwa na kilimo kisichokuwa na tija;kila mmoja anayehusika na mazao hayo atashirikishwa tutazifikia kata zetu zote kutoa elimu,"alisema Kiswaga

Ameongeza kuwa mfumo huo wa kuuza kupitia AMCOS  utawezesha kila zao kuwa na bei halisi hatua ambayo itapunguza manung'uniko  ya wakulima juu ya unyonywaji huku akiwasisitiza pembejeo bora za kilimo ikiwemo  mbolea na mbegu bora ili  waweze kuwa na kilimo chenye tija.

Sambamba na hayo aliongeza kuwa changamoto kubwa ya wakulima ni uzalishaji ,masoko na namna ya upataji wa fedha baada ya kuuza huku akibainisha kuwa mkutano huo ni mwanzo mzuri wa kuhakikisha wanawasaidia wakulima kuwa wabunifu kwa kujua wanazalisha nini kwa kiasi gani na uchaguzi sahihi wa mbegu ,matumizi sahihi ya mbolea na viuadudu.

Kwa upande wake Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika upande wa uhamasishaji, Bw. Charles Malunde  amesema  kuwa mfumo unaoweza kuwanufaisha wakulima na wenye tija ni wa stakabidhi ghalani na kuwa nguvu ya ushirika inapatikana kwa jinsi wanaushirika wanavyoshirikiana.

Naye mkurugenzi wa uendeshaji soko la bidhaa (TMX), Bw. Augustino Mbulumi amesema kupitia mfumo huu wakulima watapata taarifa za soko kwa mazao yao na watapaswa kupata malipo ya mazao yao ndani ya saa 48 hivyo ni vema wakafungua akaunti benki ili kurahisisha mapokezi ya fedha zao.

Akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Melkizedeck Humbe amesema ni vema kila mmoja akatimiza wajibu wake ili mfumo huu uweze kufanikiwa huku akibainisha kuwa mfumo huo utazisaidia Halmashauri kupata takwimu sahihi na namna ya ukusanyaji mapato

Awali  akisoma tangazo la maelekezo ya serikali kuhusu  mfumo wa ununuzi wa choroko ,dengu, mbaazi, soya, na ufuta  mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Simiyu Ibrahim   Kadudu amesema tangazo hilo litaanza kutumika mwaka huu 2020 ambapo mazao hayo yatauzwa kupitia mfumo wa ushirika kwa mfumo wa minada ya vyama vikuu vya ushirika katika maeneo yao .

Aidha imedaiwa kuwa tume ya maendeleo ya ushirika kwa kushirikiana na soko la bidhaa (TMX) itaendesha minada kwa maeneo maalum kwa mazao hayo kupitia mfumo wa soko la bidhaa na taratibu zake zitabainishwa na TMX.

Wakizungumza kwa niaba ya wakulima baadhi viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika Amcos walisema kuwa ni vema watendaji wa idara ya kilimo na ushirika wakatembelea kata zote kutoa elimu kwa wakulima ili mfumo huo ufahamike kwa wote.

MWISHO.

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/03/ununuzi-wa-mazao-mchanganyiko-kupitia.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa