• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Umoja wa Makanisa Lamadi Watoa Vifaa vya Ujenzi Shule ya Sekondari Anthony Mtaka Busega

Posted on: April 1st, 2020

Umoja wa makanisa kata ya Lamadi Wilayani Busega umetoa mchango wa vifaa vya ujenzi vikiwemo mchanga na saruji  kwa awamu ya kwanza kwa.ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Anthony Mtaka iliyopo katika Kijiji cha Lukungu kata ya Lamadi.

Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewashukuru viongozi hao kwa kuona umuhimu wa kuchangia katika maendeleo ya elimu na kuahidi kuendelea kushirikiana na madhehebu ya dini wakati wote.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Busega Tano Mwera aliushukuru Umoja wa Makanisa ya Kikristo Lamadi kwa mchango wao walioutoa kwa kutambua umuhimu wa kuchangia miundombinu ya elimu na huku akiyataka madhehebu mengine na jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa jambo hilo.

Naye mwenyekiti wa makanisa ya kikristo Lamadi, Mchungaji Michael Zacharia Kaburimoja amesema kuwa waliona umuhimu wa kuchangia miundombinu ya elimu ambapo wamechangia mchanga tripu 10 na mifuko mitano ya saruji yenye thamani ya shilingi laki saba.

"Umoja wetu una jumla ya makanisa 30 ila yaliyoridhia kuchanga ni 21 na kila kanisa linamchango wake na kila tunapopokea michango tunaiwasilisha na hatujaishia hapa bado makanisa yanaendelea kuchanga," alisema Mchungaji kaburimoja

Awali akisoma taarifa kwa niaba ya wachungaji wa makanisa hayo yaliyotoa mchango Mchungaji Emmanuel Edward Fyita kutoka Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) ameiomba serikali kuona uwezekano wa kuipandisha hadhi ya shule ya sekondari Lamadi kutoka kidato cha nne hadi cha sita kutokana na ongezeko la wanafunzi wa kidato kwanza hadi cha nne kwenye kata hiyo.

Aidha, wameiomba serikali kuanzisha shule nyingine ya sekondari katika eneo la shule ya msingi lamadi ambapo bado kuna eneo kubwa lengo likiwa kuwapunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu.

"Kuna wanafunzi wanaotoka vijiji vya mbali kama mwabasabi na Mwabulugu kwenda Lukungu waishie hapa lamadi badala ya kutembea mwendo mrefu na ujenzi huu utasaidia kukabiliana na ongezeko kubwa la wanafunzi katika shule zetu zilizo ndani ya kata ya Lamadi kwa sasa" alisema mchungaji Fyita.

"Wachungaji tulio katika umoja huu tunakuahidi kuonesha njia kwa kujenga angalau chumba kimoja cha darasa," aliongeza mchungaji Fyita.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/04/umoja-wa-makanisa-lamadi-watoa-vifaa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa