• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Ujenzi wa Tawi la IFM Simiyu Utamalizika Septemba 2019: Profesa Satta

Posted on: June 17th, 2019

Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof. Tadeo Satta amewahakikisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kuwa ujenzi wa awali wa tawi la Chuo hicho mkoani Simiyu ,unatarajia kukamilika mwezi Septemba mwaka huu na kuanza kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo 2019/2020 .

Profesa Satta ameyasema hayo Juni 17, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Tawi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Simiyu katika kijiji cha Sapiwi wilaya ya Bariadi.

Profesa Satta amesema kujengwa kwa kituo hicho kipya cha mafunzo kutachangia kuongeza udahili na  kubainisha kuwa katika mpango mkakati wa chuo mwaka 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021, chuo kimejipanga kuongeza kutoa mafunzo kwa wateja wake hasa katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Simiyu inayotarajiwa kuchukua mikoa ya kanda ya ziwa mpaka Tabora.

Ameongeza kuwa azma ya chuo ni kuanza kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo 2019/2020 kuanzia ngazi ya cheti  na matarajio ni kuhamisha wanafunzi wa ngazi ya cheti na stashahada kutoka Mwanza kuja Simiyu ili Mwanza zibaki kozi za jioni wanazosoma watu wanaotoka kazini.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amempongeza Makamu Mkuu wa Chuo IFM, Prof. Tadeo Satta kwa kuwa mtendaji wa mipango aliyoipanga na kutimiza ahadi ya kuanza kujenga tawi hilo mwaka huu, huku akitoa wito kwa wananchi wote kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hosteli, migahawa na nyumba za kupangisha watumishi.

“Tawi la Chuo cha IFM linajengwa Sapiwi watu wote wanaalikwa kuchangamkia fursa na wachangamikiaji wa fursa wa kwanza ni wana Sapiwi wenyewe, tungehitaji kupata hosteli, migahawa ya chakula, maeneo ya watu kunywa vinywaji na tutawaambia TANROADS waone namna ya kuweka “stendi” maana hapa Sapiwi kitakuwa kituo kikubwa” alisisitiza Mtaka.

Aidha, Mtaka amewahakikishia viongozi wa Chuo cha IFM kuwa viongozi wa Mkoa wataendelea kushirikiana nao  katika kuhakikisha azma ya kukamilisha ujenzi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwezesha mkandarasi kufanya kazi saa 24 kwa kuhakikisha kuna ulinzi  na miundombinu ya umeme inakuwepo katika eneo la ujenzi.

Naye Mayunga Juma Mkazi wa kijiji cha Sapiwi amesema wananchi wa Sapiwi wanashukuru  uwepo wa ujenzi huo kwani umesaidia kutoa ajira na kuwawezesha kupata fedha za kujikimu kimaisha.

Kwa upande wake Msimamizi wa Ujenzi huo kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) Kagera, Baluye Mitinje ameahidi kusimamia na kuhakikisha ujenzi unafanyika usiku na mchana ili ukamilike kwa wakati.

Ujenzi wa awali wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Tawi la Sapiwi utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia tisa na sabini na moja .

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/06/ujenzi-wa-tawi-la-ifm-simiyu.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa