• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

UCSAF Wakabidhi Kompyuta Simiyu

Posted on: April 10th, 2019

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano, Dkt. Jim Yonaz amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kompyuta 100 na vifaa vingine zikiwemo printa 10, vilivyotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 220.

Makabidhiano hayo yamefanyika Aprili 09, 2019 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi na kushuhudiwa na baadhi ya Wakuu wa Taasisi za Umma, Wakuu wa shule na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bariadi.

Akikabidhi kompyuta hizo Dkt. Yonaz amewapongeza viongozi mkoani Simiyu kwa kuendelea kufanya ubunifu katika masuala mbalimbali yanayouwezesha mkoa kukua katika nyanja mbalimbali hususani katika uchumi na elimu.

Aidha, amesema Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano itaendelea kushirikiana na Mkoa wa Simiyu kuharakisha maendeleo kupitia Sayansi na Teknolojia.

" Ninaamini kompyuta hizi zitawasaidia sana wanafunzi hawa na walimu pia yapo mambo yatakayotatuliwa kupitia kompyuta hizi, ili tuweze kuleta elimu bora, tutengeneze wasomi wazuri ambao watachangia katika uchumi wa Taifa letu" alisema Dkt. Yonaz.

Akipokea kompyuta hizo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameshukuru kwa msaada huo huku akibainisha kuwa lengo la Mkoa ni kuwa mkoa ambao uko kiganjani ambao taarifa yoyote inaweza kupatikana muda wowote.

“Tungehitaji mfahamu kuwa sisi ni miongoni mwa mikoa michache sana Tanzania yenye Mpango Mkakati wa TEHAMA wa mkoa na (focus) lengo letu kama mkoa ni kuwa mkoa ambao uko kiganjani, mkoa ambao mtu ataweza kupata taarifa yoyote wakati wowote” alisema Mtaka.

Mkurugenzi Mkuu wa UCSAF, Mhandisi. Peter Ulanga amesema UCSAF kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao inaandaa mpango wa kutoa mafunzo kwa Maafisa TEHAMA ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kibunifu.

Nao walimu na wanafunzi wa shule za sekondari mkoani Simiyu wameishukuru Serikali kutoa kompyuta hizo na kueleza namna zitakavyowasaidia.

"Kompyuta hizi kwanza zitatusaidia kuwezesha mawasiliano hususani katika masuala ya intaneti kwa ajili ya kutuma na kupokea taarifa mbalimbali kwa wakati na kuchapa majaribio ya wanafunzi" Mkuu wa Shule ya Sekondari Itilima, Mwl.Flora Shimbi.

"Vifaa hivi vitasaidia sana wanafunzi kujifunzia kwa vitendo wawapo shuleni na kutafuta 'notes' za masomo mbalimbali ili waweze kujifunza" Mkuu wa Shule ya Sekondari Bariadi, Mwl.Ally Simba

"Hizi kompyuta zitatusaidia kujifunza kwa vitendo na tutaelewa zaidi kuliko kama tungesoma bila kompyuta, kila atakachokuwa anafundisha mwalimu tutakuwa tunakiona moja kwa moja" alisema Naomi Mathias Mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Bariadi.

Kompyuta hizo pamoja na vifaa vingine vimekabidhiwa kwa baadhi ya Wakuu wa Taasisi, Ofisi za wakuu wa Wilaya, Ofisi ya mkuu wa mkoa na baadhi ya wakuu wa shule za Sekondari mkoani hapa mkoani.

MWISHO.

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/04/ucsaf-wakabidhi-kompyuta-100-simiyu.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa