• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

TFDA Yatoa Msaada wa Taulo za Kike kwa Wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha Nne waliopiga Kambi za Kitaaluma Simiyu

Posted on: June 15th, 2018

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imetoa msaada wa taulo za kike katoni 210 zenye thamani ya shilingi milioni tano  na kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaalum mkoani humo, ambao wanajiandaa na mtihani wa Taifa kwa mwaka 2018.

Akizungumza na viongozi, walimu na wanafunzi wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Bariadi Mjini Bariadi, Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa, Bw. Moses Mbambe amesema msaada huo umetolewa kujibu ombi la Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alilolitoa kwa Mamlaka hiyo kuwasaidia watoto wa kike wa kidato cha nne walio kwenye kambi ya Kitaalum mkoani humo ili wawapo kambini wasome kwa utulivu na kujiamini hususani wakati wa hedhi.

“Tunakabidhi taulo hizi za kike kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo ambazo Mkuu Mkoa wa Simiyu alimuomba ili ziweze kuwasaidia watoto wa kike wa kidato cha nne walioko kwenye kambi za kitaaluma katika maeneo mabalimbali hapa mkoani katika kuwawekea mazingira mazuri ya kusoma kuwa utulivu na kujiamini wakati wa siku zao za hedhi” alisema

Aidha, Mbambe ameupongeza uongozi wa Mkoa kwa kuanzisha utaratibu wa kambi za kitaaluma na akawataka wanafunzi kuwa na ndoto, kusoma kwa bidii na kuweka mikakati ya kuwawezesha kufikia ndoto zao; huku akiwaasa kufanya vizuri katika mitihani yao ili kutoa nafasi  kwa walio nyuma yao kuwekewa utaratibu endelevu wa kambi za kitaaluma katika kuuwezesha mkoa huo kufanya vizuri kielimu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemshukuru Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi. Agnes Sitta Kijo kwa msaada taulo za kike ambao amesema utawasaidia sana watoto wa kike ambao wengi wao wamekuwa wakitumia vipande vya kanga na vitenge kujisitiri wakati wa hedhi.

"Ni wazazi wachache sana wenye uelewa kwamba binti zao wamevunja ungo na wao kama wazazi wanatakiwa kuwapa fedha ya kununulia taulo za kike kwa ajili ya kujisitiri wakati wa siku zao za hedhi, matokeo yake mtoto wa kike katika mazingira fulani anajikuta anashawishika kuingia kwenye mambo yasiyofaa kwa kupewa pedi tu na bodaboda kwa kuwa anaona huyo ndiyo boyfriend(rafiki wa kiume) mzuri" alisema Mtaka.

Kwa upande wa wanafunzi hao wameshukuru kwa msaada wa taulo hizo ambazo wamesema zitawasaidia sana kwani baadhi yao wamekuwa wakitumia vipande vya kanga, vitenge na njia nyingine za kienyeji kujihifadhi wakati wa hedhi , hivyo wamefarijika kwa msaada huo

“Tunawashukuru sana TFDA kutupa hizi taulo za kike maana wengi wetu huwa wanatumia kanga na vitenge kujisitiri, msichana akiwa hedhi halafu akatumia taulo maalum anakuwa anajiamini, anasoma kwa amani na utulivu mkubwa tofauti na atakayetumia njia za kienyeji” alisema  Magulu Deogratius kutoka Shule ya Sekondari  Bariadi.

Katika hatua nyingine walimu na wanafunzi wa shule za sekondari Bariadi, Chenge, Gudui na Somanda zote za Wilaya ya Bariadi walimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Viongozi wote kwa kuanzisha utaratibu wa kuwa na kambi za kitaaluma, ambao wamekiri umewasaidia wanafunzi kuwa na mtazamo tofauti katika masomo na wakaomba uwe endelevu.

“Utaratibu wa makambi umewasiadia sana wanafunzi wetu, kwanza wameongeza ari ya kusoma yaani hawalali, kila tunapowafundisha wamekuwa wasikivu kwa kuwa wanakiri wanapokea vitu vipya ambavyo hawakousoma shuleni kwao, tunaomba utaratibu huu uendelee maana tuaimani utawasaidia wanafunzi wetu kujiandaa vema na mitihani ya Taifa” alisema Mwalimu Zuhura Yahaya

“Tangu tumeanza kambi hii tarehe 03 Juni imetusaidia sana kuleta mabadiliko ya Kitaaluma, tunapata nafasi ya kubadilisha uzoefu wa kujibu maswali, mada ngumu tunasaidiwa na walimu wetu, tunaelekezwa namna sahihi ya kujibu maswali; naomba tukuhakikishie Mkuu wa Mkoa matokea ya mwaka 2018 yatakuwa ya mfano;  yaani binafsi naona siku hazitoshi kama itawezekana mwezi wa tisa turuhusiwe kuja kambi tena” alisema Veronica Kidana kutoka Shule ya Sekondari Chenge.

Jumla ya Kambi za kitaaluma 149 zinaendelea kwa muda wa siku 21 mwezi huu katika maeneo mbalimbali ya mkoani Simiyu,  ambapo kambi 35 ni kwa jili ya wanafunzi wa kidato cha nne na kambi 114 ni kwa shule za msingi, kwa ajili ya maandalizi ya Mitihani ya Taifa ikiwa ni moja ya mkakati wa kuondoa daraja sifuri na daraja la nne kwa kidato cha nne na kupandisha ufaulu wa darasa la saba.

MWISHO


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa saba kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu na wanafunzi wa kike walio katika Kambi ya kitaaluma Shule ya Sekondari Bariadi baada ya kupokea msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za Kitaaluma ambao umetolewa na wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) .


Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)  Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe akizungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari Bariadi, Somada, Chenge na Gudui kabla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike uliotolewa na Mamlaka hiyo kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, katika Shule ya Sekondari ya Bariadi Mjini Bariadi.


Meneja Mawasiliano wa TFDA Guadencia  Simwanza akizungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari Bariadi, Somada, Chenge na Gudui kabla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike katoni 210  uliotolewa na Mamlaka hiyo kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, katika Shule ya Sekondari ya Bariadi Mjini Bariadi ambapo shule hizo zimeweka kambi.


Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Mhe. Athony Mtaka (mwenye suti) ,Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)  Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe , Meneja Mawasiliano wa TFDA Guadencia  Simwanza na Diwani wa Viti maalum Bariadi, Mhe. Rachel Sibanda wakiwa katika picha ya pamoja wanafunzi wa Shule ya sekondari Somanda, Bariadi, Gudui na Chenge baada ya kupokea msaada wa taulo za kike katoni 210  uliotolewa na Mamlaka hiyo kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, katika Shule ya Sekondari ya Bariadi Mjini Bariadi ambapo shule hizo zimeweka kambi.

Kutoka kulia Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)  Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe na Meneja Mawasiliano wa TFDA Guadencia  Simwanza wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi (wa tano kushoto) baadhi ya walimu wa kike na wanafunzi wa Shule ya sekondari Somanda baada ya kupokea msaada wa taulo za kike katoni 210  uliotolewa na Mamlaka hiyo kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, katika Shule ya Sekondari ya Bariadi Mjini Bariadi ambapo shule hizo zimeweka kambi.



Kutoka kulia Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)  Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe na Meneja Mawasiliano wa TFDA Guadencia  Simwanza wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi (wa tano kushoto) baadhi ya walimu wa kike na wanafunzi wa Shule ya sekondari Gudui  baada ya kupokea msaada wa taulo za kike katoni 210  uliotolewa na Mamlaka hiyo kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, katika Shule ya Sekondari ya Bariadi Mjini Bariadi ambapo shule hizo zimeweka kambi.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa