• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

TARI Yachagua Viwanja vya Nanenane Simiyu Kuwa Kituo cha Uenezaji Teknolojia

Posted on: June 16th, 2020

Kituo cha utafiti wa kilimo nchini (TARI) kimechagua eneo la viwanja vya maonesho ya nane nane vilivyopo kata ya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kuwa kituo endelevu cha uenezaji wa teknolojia lengo likiwa kuwawezesha wakulima kupata huduma za kilimo kwa mwaka mzima.

Hayo yamebainishwa na Bibi. Mshaghuley Ishika kutoka TARI Dodoma kwenye kikao cha maandalizi nane nane kilichofanyika Juni 15, 2020 kwenye jengo la mkoa wa Simiyu lililopo kwenye viwanja hivyo kikwahusiaha viongozi wa Kanda ya ziwa Mashariki(Simiyu, Mra na Shinyanga).

Aidha, Ishika amesema kituo hicho kitawarahisishia wakulima kupata bidhaa zinazozalishwa kwenye Kituo hicho ambapo kwa hapa nchini huzalishwa katika vituo 17,  huku akibainisha kuwa TARI kwa kutambua hilo wameamua kuongeza eneo la vipando katika Viwanja vya Nyakabindi na kufikia hekari 3.

"Mbali na kuwa kituo endelevu cha usambazaji teknolojia kutakuwa vifaa na duka la mbegu zinazozalishwa na TARI ambazo zinapatikana katika vituo 17 hapa nchini na litamsaidia mkulima kujifunza mengi kuhusiana na kilimo; kituo hiki pia kimepatiwa mtumishi wa kudumu atakayekuwa anasambaza teknolojia kanda ya ziwa Mashariki ," amesema Ishika.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  amesema maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020  yamefikia 70% na kuongeza kuwa kwa upande wa vipando vimefikia 75%.

Wakati huo huo  Sagini amewaomba viongozi wote wanaotoka kwenye mikoa inayounda kanda ya ziwa Mashariki (Simiyu, Mara na Shinyanga) wakiwemo wakuu wa wilaya na wakurugenzi watendaji kuhudhuria kikamilifu kwenye vikao vya maandalizi ili yale wanayokubaliana wayatekeleze kwa wakati.

Akizungumzia masuala  ambayo bado yanafanyiwa kazi Sagini amesema kwa sasa kamati ya maandalizi inaendelea na ni ukarabati wa miundombinu ikiwemo maji ,barabara na umeme huku akiwaomba washiriki kutoa michango yao mapema ili kufanikisha maandalizi kwa wakati.

Awali akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Mara,Mhe.Adam Malima, Mkuu wa wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, ameuhakikishia umma kuwa Maonesho ya Nanenane mwaka 2020 yatakuwa bora zaidi na yataacha alama; kutokana na maonesho hayo  kufanyika kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki.

Katika hatua nyingine mhandisi Msafiri amezitaka halmashauri zote ambazo hazijaanza na zile ambazo maandalizi yake yanaenda taratibu, kuharakisha kusimamia maandalizi hayo na kuhakikisha yanakuwa ya kuridhisha, ili wakulima watakapokwenda kujifunza waone umuhimu wa kilimo chenye tija.

Kanda ya ziwa Mashariki inaundwa na mikoa mitatu ambayo ni Mara, Shinyanga na Simiyu na  mwenyeji wa maonesho ya Nane nane kitaifa ni mkoa wa Simiyu kwa miaka mitatu mfululizo sasa, ambapo  kwa mwaka 2020 kaulimbiu ya maonesho haya ni "KWA MAENDELEO YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020”.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA BLOG  YETU YA MKOA KWA LINK HII:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/06/tari-yachagua-viwanja-vya-nanenane.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa