• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

TANROADS, TARURA Simiyu Watakiwa Kutenga Fedha Kuboresha Barabara Zinazounganisha Simiyu na Mikoa Mingine

Posted on: December 31st, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amezipongeza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Simiyu kwa kazi nzuri zinazofanya na kuzisisitiza kutenga bajeti ya kuboresha ujenzi wa Barabara zote zinazounganisha Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine ili zipitike wakati wote.

Kiswaga ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Desemba 30, 2019 mjini Bariadi ambapo amebainisha kuwa barabara zikiboreshwa zitarahisisha usafiri kwa wananchi na usafirishaji wa malighafi mbalimbali za viwanda na bidhaa zitakazozalishwa na viwanda, vinavyotarajiwa kujengwa Mwaka 2020.

“Kazi inayofanywa na TANROADS na TARURA ni kazi ambayo inatia moyo  na itakuwa na mchango mkubwa kwa viwanda vya nguo, glasi na vifaa tiba vitakavyoanzishwa mwakani; kwa maana ya material(malighafi) itakayoingia na bidhaa zitakazotengenezwa zitasafirishwa kwa urahisi,” alisema Kiswaga.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. John Mkumbo  amesema katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2019/20 kazi za matengenezo ya barabara ambazo zipo kwenye utekelezaji ni kilometa 108.12 na madaraja 14.3 sawa na 54.3% huku iliyokamilika kwa barabara kuu ni kilometa 246.52 na madaraja 19.71 sawa na 40.8%.

Kwa upande wake Mratibu wa TARURA mkoa wa Simiyu Mhandisi Dkt. Philemon Msomba amesema kuwa wametekeleza jumla ya miradi 30 ambayo tayari imekamilika yenye thamani ya shilingi 3,694,627,194 bila VAT .

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya Meatu, Dkt Joseph Chilongani amesema ni vyema wakala wa barabara nchini (TANROADS) na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini  (TARURA) kuboresha madaraja yaliyopo wilaya ya Meatu kwa kujenga madaraja ya juu badala ya yale yaliyopo sasa ambayo ni ya chini ili barabara hizo zipitike wakati wote.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Enock Yakobo aliwataka wakala hao kuweka taa kwenye maeneo ya katika ya miji ili wananchi waweze kufanya biashara zao nyakati zote ( saa 24).

Mbunge wa Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni ameshauri kuwa ni vema Serikali ikafanya marekebisho  katika mgao wa fedha za bajeti ya barabara kati ya wakala Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kutoka kwenye uwiano wa sasa,  ambapo TANROADS inapata asilimia 70 na TARURA  asilimia 30, iwe asilimia 40 kwa TARURA na asilimia 60 kwa TANROADS ili kuongeza ufanisi kwa TARURA.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/12/tanroads-tarura-simiyu-watakiwa-kutenga.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa