Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI imekabidhi masanduku 10 kutoka Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi kwa Mkoa wa Simiyu ili yatumike kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI.
Akikabidhi masanduku hayo Mkurugenzi wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amesema karibuni Wafadhili wamepunguza kwa kiasi kikubwa ufadhili katika masuala ya Ukimwi ni vema zikatumika fedha zetu wenyewe (wadau wa ndani) badala ya kutegemea Wafadhili
“ Ili Kuchangia fedha hizo Mfuko umebuni Masanduku ambayo Wananchi wanaweza kutoa michango kwa Fedha taslim, tumeleta masanduku haya 10 ikiwa ni maagizo ya Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Mhe. Kassim Majaliwa Waziri Mkuu,wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza 2019”
“ Katika maadhimisho hayo kila mkoa uliagizwa kuwa na masanduku hayo na kuhamasisha wananchi kuchangia jitihada hizi, Siku ya Ukimwi Duniani 2020 kila mkoa utatakiwa kutoa taarifa kuwa umechangia Serikali kiasi gani kupitia Mfuko wa Udhamini wa kudhibiti Ukimwi, alisema Dkt. Maboko.
Aidha, Dkt. Maboko amesema michango hiyo inaweza kuwakilishwa kwa kuchangia Moja kwa moja au kupitia AIrtel Money +255 684 909090 au kwa Viongozi kuchukua masanduku na kuhamasisha wananchi kuchangia katika ziara na matukio mbalimbali ambayo wao wanayaongoza huku akibainisha kuwa mpaka sasa fuko umeshaipatia Serikali kiasi cha shilingi 660.
Katika hatua nyingine Dkt. Maboko amefafanua kuwa katika fedha zote zinazokusanywa katika mfuko huu, asilimia 60 hutumika kwenye ununuzi wa dawa/vitendanishi, asilimia 25 hutumika kwenye kinga na asilimia 15 kwenye shughuli za bodi na Utawala.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Wa Simiyu, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Mashaka Luhamba ameshukuru TACAIDS kwa kutimiza ahadi ya kuleta masanduku hayo kama walivyoahidi kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa huku akiwahakikishia TACAIDS kuwa mkoa utatumia kila fursa kuhakikisha kuwa unawahamasisha Wananchi wa Simiyu kuchangia katika Mfuko huu.
Akieleza hali ya maambukizi ya VVU/UKIMWI katika Mkoa wa Simiyu, Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI Simiyu, Dkt.Khamis Kulemba amesema kutokana na utafiti wa Mwaka 2016-2017 ushamiri wa maambuziki ya VVU Mkoani Simiyu umefikia kiwango cha 3.9% ambayo ni chini ya 4.7% ikiwa ni kiwango cha kitaifa
“ Tunaendelea na kazi ya kuzuia maambukizi mapya kwa kuwezesha asilimia 90 watu wanatambua hali za afya zao, asilimia 90% ya wagonjwa wanatumia dawa na asilimia 90 nyingine kushusha kiwango cha virusi vya UKIMWI katika damu ya Mgonjwa ( Viral suppression)
Dkt. Kulemba ameongeza kuwa Mkoani Simiyu asilimia 91 ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wanatumia dawa za kufubaza makali ya VVU na kiwango cha maambukizi katika damu zao kimeshuka, huku akitoa wito kwa wananchi kuchangia mfuko wa kudhibiti UKIMWI kwani vita dhidi ya VVU/UKIMWI ni ya kila mmoja katika jamii.
Mfuko wa Udhamini wa kudhibiti ukimwi ulianzishwa Mwaka 2015, Kusudi la Mfuko huu ni kuchangia fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/07/tacaids-yakabidhi-masanduku-10-ya.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa