• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu Yajipanga Kudhibiti Ongezeko la Vifo vya Akina Mama Wajawazito na Watoto

Posted on: September 29th, 2018

Mkoa wa Simiyu umejipanga kuhakikisha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga vinapungua kwa kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imewekeza na kutumia gharama kubwa katika kuandaa wataalam(wakunga) wenye jukumu la kuhakikisha wanatoa huduma zitakazotoa majibu sahihi ya utatuzi wa changamoto hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga wakati akifunga mafunzo ya wakunga yanayohusu utoaji wa huduma za dharura kwa wakina mama na watoto wachanga chini ya mradi wa Mkunga Okoa Maisha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka yaliyohusisha wakunga kutoka katika Halmashauri zote sita mkoani humo.

Kiswaga amesema pamoja na kuwepo dalili za kupungua kwa vifo vya akina mama wajawazito na  watoto wachanga mkoani huo bado ipo haja ya kujitathmini ili kubaini ukubwa wa tatizo kama njia ya kulipatia ufumbuzi wa kudumu.

“ Ni kweli ukilinganisha takwimu za mwaka jana na mwaka huu zinaonyesha idadi ya vifo vinavyotokana na matatizo mbalimbali ya uzazi vimepungua, lakini naomba niwape angalizo,  tusizichukulie takwimu hizi kama kigezo cha ubora wa huduma zinazotolewa katika vituo vyetu, bali iwe chachu ya kufanya kazi kwa bidii  ili fikapo mwezi Desemba mwaka huu tuwe katika nafasi ya juu zaidi”.

Aidha Kiswaga amewaasa wahitimu wa mafunzo hayo kuhakikisha wanaitumia kikamilifu elimu waliyoipata ili iwawezeshe kukabiliana na dharula wakati wa kuwahudumia wakina mama wajawazito na watoto wachanga na kuongeza kuwa serikali haitamvumilia mkunga yeyete atakayetumia kisingizio cha aina yoyote kwa kusababisha kifo cha mama au mtoto.

Halikadhalika Kiswaga ameishukuru serikali ya Canada kupitia chama cha wakunga cha nchi hiyo CAM na kusema kuwa imefanya uamuzi sahihi wa kuisaidia Tanzania katika eneo hili nyeti la kuwajengea uwezo wataalamu hao watakaotumika kuboresha huduma za  afya ya mama na mtoto na kuahidi kuwa serikali iko tayari kupokea ushauri utakaosaidia kukabiliana na changamoto hiyo.

Kwa upande wake rais wa chama cha wakunga Tanzania TAMA  Feddy Mwanga amesema tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa mkunga mwenye mafunzo yuko katika nafasi nzuri zaidi ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili akina mama wajawazito na watoto wachanga kwa 87%.

“ Hivyo kwa sisi wakunga tunaamini hatua hiyo ni nzuri na kwamba kinachofuata sasa ni kuwahimiza wakina mama wahudhurie kliniki mapema na kwa wakati na hapa ndipo tunaweza kupima mafanikio ya mpango huu kupitia kwa wahitimu hawa tunaowakabidhi vyeti hii leo” alisema Bi Mwanga.

Akizungumza kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo yaliyobebwa na kauli mbiu ya Mkunga Okoa Maisha -Jonas Julius ameiomba Serikali kuboresha mazingira yao ya kutolea huduma ikiwemo kuwapatia nyumba za kuishi jirani na vituo vya kazi sambamba na kuwaendeleza kitaaluma ili waweze kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.

Mkoa wa Simiyu una jumla ya wakunga 500 ambapo  kupitia mpango huo jumla ya wakunga 220 wamenufaika na mafunzo hayo yanayofadhiliwa na CUSO International, Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) pamoja na Chama cha wakunga Canada (CAM) .

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/09/serikali-mkoani-simiyu-yajipanga-kuzuia.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa