• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu Yaandaa Mkakati Maalum wa Miaka Mitano wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba

Posted on: August 29th, 2019

Katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa  soko la pamba mkoa wa Simiyu umeandaa mkakati maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha zao hilo ili kujibu changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa Wadau wa Pamba uliofanyika uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,

Akifungua Mkutano huo Mtaka amesema upo umuhimu mkubwa kwa Mkoa wa Simiyu kuwa na kiwanda/viwanda vya kuongeza thamani ya zao la pamba ikiwemo viwanda vya nguo kama suluhisho la soko la pamba kwa wakulima.

“Kama hatutakuwa na viwanda vinavyoongeza thamani kwenye pamba,hata kama tukiongeza uzalishaji, itafika mahali tutatukanana tu, maana pamba itakuwa nyingi na hakuna mtu wa kukununua na wanaonunua wanajua hatuna kwa kuipeleka, kwa hiyo ni lazima tukubaliane na ndiyo maana tukasema tuje na mkakati huu unaoanza na mkulima kuanzia kwenye kulima” alisema Mtaka.

 

Aidha, Mtaka amesema ili kuwasaidia wakulima katika upatikanaji wa mikopo ni vema benki zikaweka utaratibu rafiki wa kutoa mikopo kwa wakulima huku akitoa wito kwa Benki Kuu kupitia Kurugenzi ya Sera kuandika maandiko ya miradi ya mazao ya mikakati likiwemo pamba ambayo yatasaidia katika kuyaongezea thamani mazao hayo.

Akiwasilisha mkakati huo kwa wadau wa pamba mkoani Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi wa Mipango na Uratibu Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah amesema uongezaji thamani kwenye pamba mkoani Simiyu bado liko chini; ambapo kwa sasa kinachofanyika ni kutengenisha pamba nyuzi, mbegu na kuchuja mafuta, huku akibainisha kuwa matarajio ya mkoa ni kwenda kwenye hatua nyingine zaidi ya kuchambua pamba.

Pamoja na kuongeza thamani ya zao la pamba wadau wa pamba wametoa maoni mbalimbali katika kuboresha kilimo cha Pamba ili kiwe chenye tija na kubainisha kuwa “Ili tuweze kuboresha kilimo cha pamba ni lazima teknolojia zitakazokabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, wadudu na magonjwa” alisema Epifania Temu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) Ukiriguru

“Mbegu ndiyo msingi wa tija ya pamba inayopaswa kuzalishwa kwenye soko, hivyo kwenye eneo lililokubaliwa kuzalisha mbegu kama Meatu na Igunga ginners (wenye viwanda vya kuchambua pamba) watakaokununua pamba ya eneo wapewe jukumu la kuzalisha mbegu ili kuwa na mwendelezo wa mbegu bora” alisema Mkondo Cornelius Afisa Kilimo Mkuu, Wizara ya Kilimo.

Mkurugenzi wa Miradi kutoka Gatsby Africa, Samweli Kilua ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha kila mdau anatimiza wajibu wake katika kuhakikisha mkakati huo unatekelezwa kwa ufanisi katika kuboresha kilimo cha pamba.

Akifunga kikao Katibu Tawalawa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema mkakati wa mapinduzi ya kilimo cha pamba Mkoani Simiyu utatekelezwa kwa vitendo  na akazitaka  Taasisi za fedha, viongozi na wataalam wanaosimamia wakulima, vyama vya ushirika  na wadau wengine waanze mazungumzo ili mkakati huo utakapoanza kutekelezwa kuwe na uelewa wa pamoja kwa wadau wote.

Mkutano wa kuboresha mkakati maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha pamba ulijumuisha wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba ambao ni pamoja na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Simiyu, Watalaam wa kilimo kutoka Taasisi za Utafiti wa Kilimo, Wizara ya Kilimo, Halmashauri na Mkoa, Watendaji wa Taasisi za Fedha, viongozi  wa vyama vya msingi vya ushirika.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI KWENYE BLOG YA MKOA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/08/simiyu-yaandaa-mkakati-maalum-wa-miaka.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa