Bariadi,
Halmashauri Mkoani Simiyu zimeagizwa kukamilisha kwa wakati maandalizi ya matumizi ya mfumo mpya wa ununuzi wa Umma kielektroniki NeST pamoja na kuanza mara moja kutumia mfumo huo ndani ya muda uliopangwa.
Agizo hilo limetolewa na kaimu katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw.Majuto Njanga alipohitimisha Mafunzo ya mfumo mpya wa ununuzi wa Umma kielektroniki NeST kwa wataalamu wa Halmashauri Mkoani Simiyu yaliyodumu kwa muda wa siku 4 tangu kufunguliwa kwake 21 Septemba 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu.
Kaimu Katibu Tawala Njanga amesema ni muhimu kwa Maafisa wa Halmashauri waliopatiwa mafunzo ya Mfumo wa NeST mkoani Simiyu kuhakikisha Taasisi zao zinaanza mara moja kutumia mfumo huo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwemo kutozwa faini iwapo watachelewa kutumia mfumo huo.
Amezitaka Halmashauri kuwasilisha haraka Taarifa ya utekelezaji wa matumizi ya Mfumo wa NeST kwa katibu Tawala Mkoa ifikapo 15 Septemba 2023 pamoja na kuhakikisha kuwa Elimu ya kutosha kuhusu mabadiliko haya inatolewa ipasavyo kwa Wazabuni na Wakandarasi ili wazeze kuwa na uelewa wa mfumo wa NeST.
Kwa upande wao washiriki walioshiriki mafunzo hayo wameishukuru Serikali kwa maboresho ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kielektroniki NeST ambapo wameahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa.
Mafunzo ya Mfumo mpya wa Ununuzi wa Umma Kielektroniki NeST yametolewa na Wawezeshaji 6 kutoka Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Simiyu baada ya wawezeshaji hao kushiriki mafunzo ya Siku 4 ya kuwajengea uwezo yaliyotolewa na Mamlaka ya udhibiti wa Ununuzi wa Umma Nchini PPRA jijini Dodoma.
GCO,
Simiyu -RS
25/08/2023
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA SEMINA.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa