• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu Tumejipanga Kikamilifu Kuwapokea Kidato cha Sita Kuanza Masomo Juni Mosi: Sagini

Posted on: May 23rd, 2020

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema mkoa huo umejipanga kikamilifu kuwapokea wanafunzi wa kidato cha sita kwa ajili ya kuanza masomo Juni Mosi, 2020 kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe  Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari leo 23 Mei,2020 Sagini amesema Simiyu iliandaa mkakati maalum kwa kushirikiana na wadau kuwawezesha wanafunzi kujisomea hivyo, mkoa utahakikisha muda uliotolewa na Wizara ya elimu kufanya maandalizi ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita (Juni Mosi-Juni 28) unatumika vizuri na walimu na wanafunzi kwa ajili ya rejea na kukamilisha mada.

“Sisi kama mkoa elimu ni kipaumbele cha kwanza  hivyo tumejipanga kikamilifu kuwapokea vijana wetu wa kidato cha sita, ikumbukwe pia kuwa kama mkoa tuliandaa mkakati wa kuwasaidia wanafunzi kujisomea hususani madarasa ya mitihani wakati walipokuwa likizo ya tahadhari ya Corona; tutahakikisha muda uliotolewa na wizara ya elimu kujiandaa na mtihani wa Taifa unatumika vizuri kufanya marejeo na kukamilisha mada zilizobaki,”alisema Sagini.

Aidha, Sagini amesema viongozi katika maeneo yote watahakikisha tahadhari zote zinazotolewa na Wizara yenye dhamana na Afya katika  kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona zinazingatiwa katika shule zote za kidato cha sita Mkoani Simiyu katika kipindi chote watakachokuwepo shuleni.

Vile vile Sagini ametoa wito kwa wazazi na walezi mkoani Simiyu kuendelea kuwahimiza na kuwasimamia watoto wao walioko majumbani kujisomea wakati huu ambao wengine bado wako likizo mpaka shule zitakapofunguliwa, huku akisisitiza kuwa mkakati wa mkoa wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wakiwa likizo utaendelea kutekelezwa.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema pamoja na utekelezaji wa mkakati maalum wakati likizo, kabla ya serikali kutangaza kufunga shule wanafunzi wa kidato cha sita walikuwa katika kambi ya kitaaluma, ambapo takribani mada zote zilikuwa zimeshakamilika na wanafunzi walikuwa wakipewa majaribio na kurudia mada ambazo hazikueleweka vizuri.

Naye  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza amesema  idara ya elimu katika Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na waratibu elimu kata  wamejipanga kuhakikisha kuwa wanakamilisha mahitaji yote ya kujisomea kwa wanafunzi wa kidato cha sita yanaandaliwa na kukamilika kwa wakati ili kuwawezesha kujiandaa na mtihani wa Taifa.

Kwa upande wake mmoja wa wazazi wenye wanafunzi wa kidato cha Sita mjini Bariadi, Bw. Chambwite Sadala amesema anaunga mkono uamuzi wa Mhe. Rais wa wanafunzi wa kidato cha sita kurudi shuleni, hivyo akatoa wito kwa wanafunzi hao kwenda kufanya bidii katika kujisomea katika muda waliopewa ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kufikia malengo yao.

Mkoa wa Simiyu una jumla ya shule 13 za sekondari za Kidato cha tano na Sita, ambapo kwa mwaka 2020 jumla ya wanafunzi 953 wa kidato cha Sita wanatarajiwa kufanya mtihani wa Taifa kuanzia tarehe 29 Juni 2020 kama ilivyotangazwa na Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako.

MWISHO

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa ufafanuzi wa jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)  Mei 23, 2020 kuhusu utayari wa mkoa katika kuwapokea wanafunzi wa kidato cha sita kuanza masomo Juni Mosi, 2020 kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa