• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu Kuvuna Pamba Kilo Milioni 300 mwaka 2018

Posted on: February 14th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema mkoa huo unatarajia kuvuna kilo milioni 300 za zao la pamba katika msimu wa mwaka 2017/2018

Mtaka aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Bariadi Mjini katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mnada wa Kidinda.

 “ Matarajio yetu mwaka huu kama mkoa ni kuvuna pamba ambayo haijawahi kutokea tangu tumepata Uhuru, ndiyo maana  tunafuata vinyunyizi(dawa za kuuwa wadudu) chupa milioni mbili, tunatarajia kuvuna zaidi ya kilo milioni 300 za pamba” alisema Mtaka.

Amesema kutokana ongezeko hilo la mavuno matarajio ya Mkoa ni kuongezeka kwa mzunguko wa fedha ndani ya mkoa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa vibarua na wafanyakazi katika Viwanda vya kuchambua pamba(ginneries).

Aliongeza kuwa Serikali ina mpango wa kujenga Kiwanda cha bidhaa za Afya zitokanazo na zao la pamba katika Mkoa wa Simiyu ambacho kitaajiri zaidi ya watu 3000 hivyo akawataka wananchi kuzitumia fursa hizo vizuri.

Aidha, Mtaka alisema Mkoa unaandaa utaratibu wa kuwawezesha wafanyabiashara hasa katika siku za Minada ya Bariadi mjini(Kidinda) na Dutwa (Jumanne na Alhamisi) kufanya biashara kwa masaa sita zaidi, kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 06:00 usiku katika moja ya barabara za Mjini Bariadi.

Alisema barabara hizo zitawekewa taa na Uongozi wa Mkoa na Wilaya utazungumza na Jeshi la polisi namna ya kufanya Doria ili kuwahakikishia  wafanyabiashara hao usalama wao na mali zao.


Wakati huo huo Mtaka amewaeleza wananchi wa Wilaya ya Bariadi kuwa Mkoa wa Simiyu umepata Kanda ya Simiyu ya Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane nane itakayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga , ambapo Uwanja wa Maonesho unatarajiwa kujengwa katika Mtaa wa Nayakabindi Halmashauri ya Mji wa Briadi 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mhe.Robert Lweyo alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa jitihada anazofanya katika kuwaletea maendeleo wananchi, ikiwa ni pamoja na kusimamia suala la Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda ambapo alimshukuru kwa kutafuta vyerehani 50 ambavyo vitatumika kuanzisha kiwanda cha ushonaji.

Katika Mkutano huo wa Hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mnada wa Kidinda wananchi walitoa kero zao ambazo zote zilipatiwa majawabu na viongozi na Wataalam ngazi ya Wilaya ya Mkoa.

MWISHO 

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA TUKIO HILI FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/02/simiyu-kuvuna-pamba-kilo-milioni-300-za.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa