• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu Kutumia Mabweni Shule za Sekondari Kuhifadhi Washukiwa Maambukizi ya CORONA

Posted on: April 1st, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa umetenga shule za Sekondari za Bweni za Serikali kuwa maeneo ambayo yatatumika kuwahifadhi washukiwa wa Virusi vya Corona endapo watapatikana mkoani hapa; baada ya serikali kufunga shule na vyuo nchini kwa siku 30 lengo likiwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Mhe. Mtaka ameyasema hayo wakati akipokea mchango kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Anthony Mtaka uliotolewa na umoja wa Makanisa Lamadi na kuongeza kuwa mbali na maeneo ya shule Mkoa pia umetenga maeneo ya hoteli ambayo yatatumika endapo washukiwa/watu wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huo ambao hawatahitaji kukaa kwenye maeneo ya shule.

"Mkoa hautatumia hoteli kwa ajili ya kuhifadhi mtu yeyote atakayeshukiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona badala yake tutatumia shule za zetu za sekondari za bweni lakini ikitokea mtu anahitaji kukaa hotelini tayari tumeandaa hoteli za kutosha,"alisema Mtaka.

" Tumechukua uamuzi huu ili kuwapunguzia watakaoshukiwa kuwa na ugonjwa huo gharama ila utaratibu huu hautawafunga watu wenye uwezo ambao watapenda kwenda hotelini; kwa mara nyingine tena niwaombe wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na viongozi kuzuia maambukizi ya CORONA," aliongeza Mtaka

Hata hivyo aliongeza kuwa tayari kila wilaya imetenga shule yenye vitanda vya kutosha na mazingira mazuri kwa ajili ya washukiwa wa ugonjwa huo, huku akiwataka wananchi wa mkoa huo kuendelea kuchukua tahadhari.

Mbali na hayo amewataka wazazi wa wanafunzi wa madarasa ya mitihani mkoani humo kuhakikisha wanawasimamia watoto wao wanajisomea katika wa kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kutokana na ugonjwa huo.

MWISHO

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa