Katika kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana mkoa wa Simiyu umejipanga kufanya majaribio ya kutumia vyeti vya taaluma kwa wahitimu wa vyuo vikuu kama dhamana ya mikopo ili kuwawezesha kupata mitaji na kujiajiri kupitia sekta ya kilimo na viwanda.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alipokutana na baadhi ya vijana jana Novemba 15, 2020 mjini Bariadi kwenye mjadala wa ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo ambao ulihudhuriwa pia na wadau wa maendeleo akiwemo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP), Bibi. Christine Musisi.
“Tunataka (tu pilot) tufanye majaribio na tutakuwa (number one) wa kwanza, tutawafuata wadau (UNDP) kuwaeleza kuwa tumekuja na namna ya kuwasaidia vijana waliomaliza vyuo vikuu ili tuone kama vyeti vyao vinaweza kusimama kama dhamana badala ya vyumba na viwanja ambavyo wao hawana,”
“Tutawaambia vijana hao wenye maandiko ya miradi wawasilishe iwe ni kwa mtu binafsi au kikundi, tutajadiliana tuone ‘risk’ zikoje,” alisema Mtaka.
Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bibi. Christine Musisi ametoa wito kwa vijana kuhamasika kubadili mitazamo kutoka kwenye mawazo tegemezi kwenda katika mawazo ya kujitegemea wenyewe na kwenda mbele zaidi kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka, huku akiahidi kuwa UNDP itaendelea kushirikiana na Mkoa wa Simiyu kama mdau wa maendeleo.
Baadhi ya vijana wametoa mapendekezo mbalimbali ambayo yakifanyiwa kazi na serikali, vijana wenyewe na wadau wengine yataweza kuchangia kuleta ufumbuzi wa tatizo la ajira kwa vijana.
“Tunaomba Serikali ituboreshee miundombinu ya kilimo tutoke kwenye kilimo cha kutegemea mvua twende kwenye kilimo cha umwagiliaji ili tuzalishe malighafi ya kupeleka viwandani,” alisema Adrian Paul.
“Njia nyingine ya kuongeza ajira kwa vijana na Serikali kufufua viwanda vilivyokufa na kuanzisha viwanda vipya ili iweze kuzalisha ajira kwa rika zote wakiwemo vijana,” alisema Afisa Vijana Itilima
“Elimu ya kujitegemea irudishwe na ianze kufundisha mashuleni ili kuwaanda watoto tangu wakiwa wadogo kujitegemea ili hata atakapomaliza masomo akakasa ajira aweze kujiajiri mwenye na kujitegemea,” alisema Asia Kimaro kutoka Wilayani Maswa.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka UNDP, Bw. Amon Manyama ameahidi kushirikiana na mkoa wa Simiyu katika maandiko ya miradi huku akitoa wito kwa vijana kujituma na kutokuridhika kwa kufanya kazi moja badala yake kila mmoja aone umuhimu wa kuwa kazi zaidi ya mbili.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/11/mkuu-wa-mkoawa-simiyu-mhe.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa