Serikali mkoani Simiyu kwa kushirikiana na wadau Shirika liliso la kiserikali la InterHelath imeanzisha huduma ya tohara kinga kwa watoto wachanga na tayari zoezi hilo limekwishaanza wilaya ya Meatu ambapo wataalam wanaotoa huduma hiyo wamekwishapatiwa mafunzo.
Matarajio ya serikali ni kusambaza huduma hiyo ya tohara kinga kwa watoto wachanga kwenye wilaya zote mkoani hapo ili huduma hiyo ipatikane kiurahisi na kwa wakati na kulifanya zoezi hili kuwa utamaduni ili jamii ione umuhimu wake tangu mtoto akiwa mdogo .
Hayo yamesemwa na mratibu wa kudhibiti UKIMWI mkoa wa Simiyu Dkt Khamis Kulemba Julai 12, 2019 wakati akiongea na waandishi wa habari katika mahojiano maalum matra baada ya kuhitimishwa kwa kikao cha wadau wa AFya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Ameongeza kuwa awali zoezi la tohara lilikuwa la hiari kwa wanaume waliokuwa bado hawajafanyiwa huduma hiyo ambapo amesema lilipokelewa kwa mwititiko mkubwa hivyo ikaonekana ipo haja na umuhimu wa kutoa huduma hiyo tangu mtoto akiwa mdogo ili kuwa na kizazi kijacho kilichopata huduma hiyo .
“kwa kipindi cha mwaka 2017/18 mpango wa tohara ya hiari kwa wanaume ulijikita katika halmashauri ya Bariadi, halmashauri ya Itilima na halmashauri ya Meatu kama mkoa tulikuwa tunataka tutoe tohara kinga kwa wanaume takribani 59,129 kuanzia Oktobar 2018 na kila halmashauri ina lengo lake kwa kwa Bariadi lengo lilikuwa kutahiri zaidi ya wanaume 20,440 lakini tulifanikiwa kutahiri wanaume 17,165 sawasawa na 84%, alisema Dkt Kulemba na kuongeza kuwa:
“kwa wilaya ya Itilima lengo lilikuwa kuwafikia kina baba wapatao 22,176 lakini mpaka tarehe 30 june tuliwafikia wanaume 16,621 sawasawa na asilimia 75 , kwa wilaya ya Meatu tumekwenda mbali kidogo lengo la lilikuwa kuwafikia wanaume 16,513 na mpaka mwisho wa mwezi wa sita tarehe 30 tumewafikia wanaume 15,165 sawasawa na 92% kwa mkoa mzima tumeshawafikia wanaume 48,951 sawa na 82% aliongeza Dkt Kulemba”
Aidha Dkt Kulemba ameongeza kuwa kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika nchini Kenya ,Uganda na Afrika Kusini maeneo mengi ambayo tohara kwa wanaume ni utamaduni wao maambukizi ya UKIMWI yapo chini ikilinganishwa na maeneo ambayo tohara ipo chini maambukizi yapo juu.
“maeneo ambayo tohara ni culture(utamaduni) yao maambukizi ya virusi vya ukimwi yapo chini lakini kupitia wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika la Interhealth hayo yote yameweza kufanyika na ndio maana tukapata matokeo haya ” alisema Dkt Kulemba .
MWISHO.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa