Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali itahakikisha maeneo yote yanayozunguza Ziwa Victoria yanapata maji safi na salama ili kuwaondolea adha wananchi wa maeneo hayo ambayo yanazungukwa na rasimali hiyo muhimu.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Lamadi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji wa Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu, ambao umegharimu shilingi bilioni 12.8 fedha ambazo ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Ufaransa na Benki ya Uwekezaji ya Jumuiya ya Ulaya.
“Tumeamua Serikali ya Awamu ya Tano kuanza mpango wa kuhakikisha miji yote iliyo kando kando ya Ziwa Victoria inapata maji na ndiyo maana Lamadi mmepaa maji hongereni sana; mradi huu utatoa lita milioni 3.3 kwa siku mahitaji ya maji ya hapa ni lita milioni 1.8 kwa hiyo ni maji mengi yatakuwa yanatoka kwa siku kuliko mahitaji” alisema Rais Magufuli.
Aidha, amewataka Wananchi wa Wilaya ya Busega kuutunza mradi huo na akawaonya kuwa endapo watahujumu miundombinu na kuuharibu serikali haitapeleka mradi mwingine.
Naye Waziri wa maji na Umwagiliaji, Mhe. Makame Mbarawa amesema mradi huo utakapo kamilika mwezi Mei 2018 utawahudumia zaidi ya watu laki tatu watapa maji safi na salama.
Prof. Makame Mbalawa amesema ili kuondokana na changamoto ya maji katika Mkoa wa Simiyu Serikali imekusudia kutekeleza mradi mkubwa wa Maji kutoka Ziwa Victoria utakaowanufaisha wananchi wa Wilaya ya Bariadi,Itilima na Mwanhuzi Meatu, ambao utagharimu shilingi bilioni 378.
Pamoja na kuweka Jiwe la Msingi, Mhe. Rais Magufuli pia amefungua Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Kufungua Mtandao wa barabara za lami Mjini Bariadi zilizojengwa chini ya mradi wa ULGSP na kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Bariadi-Maswa inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye refu wa KM 49.7.
Sepemba 09, 2018 Mhe. Rais Magufuli anaendelea na ziara mkoani Simiyu ambapo atapita na kufanya mkutano wa hadhara Lagangabilili Itilima na kuelekea Meatu.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/09/serikali-yawahakikishia-wananchi.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa