• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Serikali Yawahakikishia Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu Bariadi Kupewa Leseni

Posted on: November 24th, 2020

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila amewahakikishia wachimbaji wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Bulumbaka uliopo katika kijijj cha Gasuma wilayani Bariadi mkoani hapa kuwa watapata leseni za uchimbaji na kusisitiza kuwa kamwe hawataondolewa katika mgodi huo.

Prof. Msanjila ameyasema hayo jana Novemba 23, 2020 wakati akizungumza katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi na baadhi ya wachimbaji wadogo, katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

"Muombe leseni mtapewa, leseni haiwezi kutolewa kwa mtu kutoka huko aliko halafu hawa vijana ambao wanachimba sasa hivi wakaondolewa hapana; najua kuna maombi nayaonaona kwenye mitandao lakini msiwe na wasiwasi hayawezi kutoka," alisema Prof. Msanjila.

Aidha, Prof. Msanjila ameeleza utaratibu wa fidia kwa wenye mashamba "tusiichukulie kwamba kwa kuwa na shamba unakuwa na haki ya kuchimba, hapana; ila ni kwamba wale wanaochimba hawana fedha ya kukufidia, sasa  tumeweka utaratibu kwamba fidia yako uipate taratibu kwenye mgao na naamini huwa ni nyingi kuliko fidia nyingine.”

Katika hatua nyingine Prof. Msanjila amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kuanzisha upya mchakato wa kumpata msimamizi wa mgodi wa Bulu90a mbaka ambaye atahakikisha ulinzi unaimarishwa, mazingira yanaboreshwa ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa vyoo pamoja na kuimarisha uhusiano mzuri miongoni mwa wachimbaji

Awali baadhi ya wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba walisilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili katika mgodi huo ikiwa ni pamoja na kuomba uboreshaji wa miundombinu na upatikanaji wa huduma muhimu, ambapo Msanjila amebainisha kwamba Serikali inazifanyia kazi na baadhi zitatatuliwa na msimamizi wa mgodi huo baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata ambao utaanzishwa Mkuu wa Wilaya.

“Wachimbaji tumewekeza gharama kubwa sana, tunaomba serikali isaidie kuimarisha ulinzi na usimamizi wa mali tunazochimba na kuendelea kuboresha miundombinu ili tuweze kusafirisha mali tunazochimba hapa kwa urahisi,” alisema mchimbaji mdogo, Bw. Wibelo Kihalata.

“Wenye Maeneo tuliomba leseni ili na sisi tuweze kufanya kazi na Watanzania wenzetu, tunashukuru kwa kuwa mmetueleza kuwa hata sisi tukijiunga tunaweza kupata leseni tukachimba na siyo wenye hela peke yao tu,” alisema Masuke Sahani Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja Bulumbaka Bariadi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema  atahakikisha mchakato wa kumpata msimamizi wa mgodi linafanyika kwa uwazi na kusimamia uendeshaji wa mgodi huo kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo  kutoka wizara ya Madini.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga amesema Serikali ya mkoa wakati wowote itahakikisha inasimamia Serikali ya wilaya katika kuhakikisha shughuli zote zinazofanyika zinafuata sheria, kanuni na taratibu.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/11/serikali-yawahakikishia-wachimbaji.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa