• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Serikali Yatoa Vitabu 297,891 kwa Shule za Msingi Mkoani Simiyu

Posted on: May 5th, 2018

Serikali imetoa jumla ya Vitabu 297, 891 kwa ajili ya wanafunzi wa Shule za Msingi wa Darasa la kwanza mpaka darasa la Tatu Mkoani Simiyu

Akizungumza kabla ya makabidhiano ya vitabu hivyo Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Ndabazi Stephano amesema vitabu hivyo vitakidhi mahitaji ya wanafunzi kwa kuwa idadi yake ni kubwa zaidi ya idadi ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu ambao wako 261,257 kwa mkoa mzima.

Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila shule ina vitabu vinavyojitosheleza na inaendelea kuchapisha vitabu vya darasa la nne, ambapo Ofisi ya Rais TAMISEMI imeanza kugawa vitabu hivyo katika mikoa mbalimbali na akabainisha kuwa mkoa wa Simiyu nao utapewa vitabu hivyo.

"Tunaendelea kugawa vitabu vya darasa la nne katika mikoa mbalimbali hapa nchini, hadi sasa vimegawanywa katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Dodoma, Morogoro na awamu inayokuja ni Mikoa ya Kanda ya Ziwa ukiwemo Simiyu” alisema Stephano.

“Vitabu hivi ni original (halisi) kabisa hamna kitabu feki hapa, maana kuna taarifa zinasambaa mitandaoni kuwa vitabu hivi vimekosewa, niwaeleze walimu na wanafunzi mliopo hapa vitabu hivi tunavyovigawa ni halisi na havijakosewa” alisisitiza Ndabazi Stephano

Aidha, Bw. Gaitan Romwald kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) amesema vitabu hivi vinagawiwa kwa awamu, hivyo vipo vitabu vingine vya darasa la kwanza mpaka la tatu ambavyo kwa Mkoa wa Simiyu vitagawiwa pamoja na vitabu vya darasa la nne awamu ijayo.

Akizungumza na walimu na wanafunzi walioshuhudia makabidhiano ya vitabu hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewataka wanafunzi kuvitunza na kuvisoma ili viwasaidie katika masomo yao, huku akiwataka walimu kuvitumia vitabu hivyo kuwafundisha wanafunzi kwa moyo.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory ameishukuru Serikali kwa kuleta vitabu hivyo ambavyo amesema vitatatua tatizo la upungufu wa vitabu uliokuwepo kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaoandikishwa mwaka hadi mwaka.

Walimu na wanafunzi pia wameishukuru Serikali kwa kupeleka vitabu hivyo Mkoani Simiyu ambavyo vitakuwa chachu na njia mojawapo ya kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kuleta hivi vitabu, vitatusaidia katika masomo yetu maana tutajisomea ili tujifunze na kupata uelewa zaidi" Eliasi John mwanafunzi Shule ya Msingi Somanda A

“Kwa niaba ya walimu wenzangu na wanafunzi wetu, napenda kuishukuru Serikali kutuletea vitabu hivi, vitakuwa msaada mkubwa sana kwa wanafunzi wetu lakini hata kwetu pia na vitatusaidia sana kuboresha mazingira yetu ya kufundishia watoto” Mwalimu Janeroza Gabriel

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/05/serikali-yatoa-vitabu-297891-kwa-shule.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa