• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Serikali Yaondoa Zuio la Kuuza Mazao Nje ya Nchi

Posted on: August 8th, 2018


Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa amesema Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi  ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini.

Mhe. Mkapa amesema hayo katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu,  Uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi ambapo alikuwa mgeni Rasmi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

“Ninachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi    ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini, hata hivyo mazao hayo yatauzwa nje ya nchi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu”alisema.

 

Aidha,  amesema Serikali inawakumbusha wananchi wote kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula wakati wa kuuza mazao yao ili kujihakikishia usalama wa chakula katika kaya zao.

Mkapa pia amesema Serikali ina mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la pamba kutoka tani 121,000 mwaka 2016/2018 hadi kufikia tani milioni moja mwaka  2020.

Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba ametangaza rasmi kuwa Maonesho ya Nane nane Kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo hadi mwaka 2020 yatafanyika kanda mpya  Kanda ya Ziwa Mashariki katika Uwanja wa Nyakabindi Bariadi, huku akisisitiza kuwa maonesho hayo yafanyike Kimataifa kwa kushirikisha nchi jirani zinazoizunguka Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema  Mkoa wa Simiyu utaendelea  kulipa kiupaumbele zao la Pamba na mwaka ujao uzalishaji utaongezeka kutoka kilo milioni 70 hadi kufikia kilo 150.

“Simiyu tunajivunia wananchi wachapa kazi wenye uthubutu na Simiyu inajengwa na Wanasimiyu, mwaka jana tumezalisha kilo milioni 70 za pamba, kwa mwaka huu sasa hivi msimu ukiwa umefikia katikati tuna kilo milioni 85, mwakani tunatarajia kuzalisha kilo zaidi ya 150” alisema

Ameongeza kuwa wananchi wamelima chakula cha kuwatosheleza si watu wa kuomba chakula cha msaada huku akiupambanua Mkoa wa Simiyu kuwa ni mkoa pekee ambao watu wake wanafanya biashara saa 24.

Maonesho ya Nanenane Mwaka 2018 yaliwashindanisha wakulima na wafugaji mmoja mmoja, Taasisi, Wakala, Mashirika ya Umma na Binafsi, Wizara pamoja na Halmashauri 21 za Mikoa ya Simiyu Mara na Shinyanga ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imekuwa ya tatu kati ya hizo 21.

Kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2018 “ WEKEZA KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA”

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:https://simiyuregion.blogspot.com/2018/08/serikali-yaondoa-zuio-la-kuuza-mazao.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa