• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Serikali Yaanza Maandalizi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Mwanza-Isaka, Bandari Kavu Kujengwa Simiyu

Posted on: March 9th, 2021

Serikali imeanza maandalizi ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka yenye urefu wa kilomita 341 ambayo itajengwa kwa gharama ya shilingi trilioni 3.0267 fedha za ndani, ambapo katika mradi huu Bandari kavu na stesheni  vinatarajiwa kujengwa katika eneo la Malampaka wilayani Maswa mkoani Simiyu..

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa Machi 08, 2021 katika kikao cha pamoja cha wadau ambacho kilifanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya utekelezaji wa mradi huu ili  kufanya maandalizi muhimu.

“Hapa Malampaka tutakuwa na kambi ya watu zaidi ya 3000 kwa hiyo ni vizuri wananchi wakaandaliwa ili waweze kushiriki fursa mbalimbali, tunatarajia pia kujenga bandari kavu kama ilivyo Isaka mizigo kutoka mikoa mbalimbali itaishia hapa; Malampaka pia tutajenga stesheni jengo kubwa lenye mita za mraba 8000 ambayo ndani itakuwa na benki, maduka na huduma nyingine,” alisema Kadogosa.

“Mradi huu ni lazima uwe na maana kwa maisha ya watu wa kawaida, mahitaji mbalimbali yatahitajika na watenda kazi kwenye mradi huu kama vile malazi, chakula mfano kuku tu zitahitaji zaidi ya kuku 40,000 kwa mwezi, kwa hiyo hii ni fursa nzuri itakayobadilisha maisha ya wengi, wananchi wajipange kutumia fursa hii,” alisisitiza.

Aidha, Kadogosa ametoa wito kwa wananchi na wadau wengine kutoka taasisi mbalimbali kushirikiana na TRC ili utekelezaji wa mradi huu usiathiri shughuli mbalimbali za wananchi na taasisi hizo zinazotoa huduma kwa jamii, huku akiahidi kuwa TRC itaendelea kusimamia upatikanaji wa fursa zipatikane kwa usawa kama ilivyoelekezwa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa wa Simiyu umepokea mradi huo kwa asilimia 100 na kuahidi kutoa ushirikiano, huku akiwahakikishia usalama wakandarasi na watu wote watakaohusika na utekelezaji wa mradi huu.

Kiswaga ameagiza idara ya ardhi Maswa kupima maeneo ili wananchi waweze kupata maeneo ya kujenga na kuwekeza kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali, ambapo pia ametoa wito kwa wananchi kununua maeneo hayo yatakapotangazwa, ili waweze kujenga nyumba za kuishi na kuwekeza katika fursa mbalimbali kuinua uchumi wao, mkoa na Taifa kwa ujumla.

Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu, Bi. Haula Kachwamba ametoa wito kwa Wananchi wa Malampaka kila mmoja kuwa mlinzi wa mali za mkandarasi na serikali, “ Hatutegemei mali ya serikali na mkandarasi ikaibiwa, tunategemea itafanya kazi iliyokusudiwa hivyo kila mmoja akawe mlinzi, lakini pia mjiandae kutumia fursa hii, wakulima, wafugaji, mama ntilie kila mmoja kwa namna yake.”

Mwenyekiti Kijiji cha Ikungu Bw. Chuma Gashi amesema wananchi wa Kijiji hicho wameupokea mradi huo kwa mikono miwili na wako tayari kupisha maeneo yatakayohitajika kwa kufuata taratibu huku akibainisha kuwa yeye binafsi kama mwananchi amejipanga kufanya biashara ya kuku katika kambi itakayojengwa Malampaka na baadaye reli ikikamilika atasafirisha kwenda Dar es salaam.

Naye Julia Musa amesema “mradi wa reli tumeupokea kwa furaha maana tunajua mji wetu wa Malampaka utapata maendeleo, vijana watapata ajira, tunamuombea Mhe. Rais azidi kutuletea miradi mingine ili sisi wana Malampaka tuzidi kupata maendeleo, tuko tayari kupisha mradi na kwenda kwenye maeneo tutakayopangiwa na serikali tukilipwa fidia ili kupisha ujenzi wa reli hii.”

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Aswege Kaminyoge amesema eneo la Malampaka linakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 14,300.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KUNGANISHIHIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2021/03/serikali-yaanza-maandalizi-ujenzi-wa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa