• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Serikali Kutaifisha Pamba itakayonunuliwa Nje ya Mfumo wa Vyama vya Ushirika Vya Msingi

Posted on: May 3rd, 2018

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba nchini Marco Mtunga amewaonya wanunuzi wa Pamba watakaonunua pamba nje ya mfumo wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) na kuwa endapo watabainika Pamba hiyo itataifishwa na Serikali.

Onyo hilo limetolewa Mkoani Simiyu katika kikao baina ya Viongozi wa mkoa huo, viongozi wa vyama vya ushirika vya Msingi (AMCOS), wanunuzi wa Pamba na Naibu Mrajisi  kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dodoma Charles Malunde, lengo likiwa ni kukumbusha juu ya uadilifu katika masuala ya ununuzi wa pamba, ikiwa ni maandalizi wa ununuzi pamba baada ya msimu kufunguliwa.

Mtunga amesema mwaka huu Serikali imefanya uamuzi kwamba pamba yote itakayozalishwa hapa nchini itanunuliwa kupitia Vyama vya Msingi (AMCOS) jambo ambalo amesema limeelezwa vizuri katika mwongozo wa bodi.

“Tunawatahadharisha wanunuzi wa pamba kufuata mfumo wa ununuzi wa pamba uliowekwa na Serikali, pamba yote itakayokamatwa ikiwa haikununuliwa kupitia Chama cha Ushirika cha Msingi itataifishwa na Serikali,  katika mwongozo tulioutoa maelekezo hayo yapo na yako chini ya sheria Namba 2 ya pamba ya mwaka 2001” alisema Mtunga.

Kwa upande wake Naibu Mrajisi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dodoma Charles Malunde amewataka viongozi wa Vyama vya ushirika kuepuka aina yoyote ya wizi na ubadhilifu wa kutumia udanganyifu wa kuwaibia wakulima kwa kuziharibu mizania.

Aidha, Malunde amesisitiza sheria na taratibu za Ushirika zizingatiwe katika uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi, hivyo akawataka viongozi wote waliochaguliwa kuongoza vyama hivyo ambao wana shutuma zozote, watumishi wa Umma au Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa kuachia mara moja nafasi hizo kwa kuwa hawana sifa kwa mujibu wa sheria.

Baadhi ya viongozi wa AMCOS waliwasilisha masuala mbalimbali kama maombi yao kwa Serikali kuhusiana na ununuzi wa pamba ikiwa ni pamoja na kuomba vyama vya ushirika vya msingi vipya vilivyo  katika hatua ya usajili vikamilishiwe usajili ili viweze kuingia katika mfumo huu wa ununuzi wa pamba.

Akihitimisha kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema anatamani kuona ushirika wenye mtazamo wa kujibu changamoto na mahitaji ya wakulima wa pamba, huku akitoa angalizo kwa viongozi wa AMCOS watakaofanya ubadhilifu wa fedha za Vyama vya Ushirika kuwa Serikali mkoani humo itawachukulia hatua kali.

“Ushirika wa Simiyu (is my own baby) ni mtoto wangu mwenyewe, ni kitu ambacho nilitamani kuona kinatokea, Wanaushirika wakakaokosa uadilifu wajihesabu kuwa wafungwa watarajiwa, nawaambia nitawafunga na sitanii nitawafunga” alisisitiza Mtaka.

Katika hatua nyingine amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kuaandaa eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya Chama Kikuu cha Ushirika Simiyu.

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/05/serikali-kutaifisha-pamba.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa