Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa Serikali mkoani hapa kuilea na kuipenda sekta binafsi na kuona namna sahihi ya kutatua changamoto zinazoikabili badala ya kufikiria namna ya kukusanya mapato tu kutoka katika sekta hiyo.
Mtaka ameyasema hayo katika kikao maalum cha kujadili Hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambapo Halmashauri ya Mji Bariadi na nyingine za Mkoa wa Simiyu pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa. Simiyu zimepata hati safi.
“Viongozi wa Serikali tujifunze kuilea sekta binafsi, sekta binafsi ni lazima ilelewe na ipendwe pia, tuone namna ya kutatua changamoto zinazoikabili na kuwafanya watu wapende kufanya biashara badala ya kufikiria kukusanya mapato tu,” alisema Mtaka.
Mtaka ametoa wito huo kutokana na mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti ya CAG kuwa pamoja na Halmashauri ya Mji Bariadi kupata hati safi, iko haja kwa Halmashauri hiyo kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na Usimamizi wa Mapato yatokanayo na vyanzo vya ndani, huku akisistiza kuweka utaratibu mzuri wa utoaji wa mikopo ya wanawake, vijana na wenye ulemavu kutoka katika asilimia 10 ya mapato hayo ya ndani.
Aidha, Mtaka amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha wanawalipa madiwani stahili zao kabla ya muda wao kuisha (kabla ya mabaraza ya amadiwani kuvunjwa, “tusingehitaji tuvunje mabaraza madiwani wetu wakiwa wanadai stahili zao, Wakurugenzi wote hili liwe kipaumbele chenu.”
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa