Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt.Yahaya Nawanda Juni 6, 2023 amezindua rasmi Mfumo wa kurahisisha usafiri wa dharura kwa Wajawazito,waliojifungua na watoto wachanga Mkoani Simiyu.
Akizingumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo huo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Dkt Nawanda amesema Mfumo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo kwa akina mama na watoto wachanga kutokana na changamoto za uzazi.
Dkt.Nawanda amewapongeza Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,pamoja na wadau wa Mfumo wa M-Mama kwa kushirikiana vema na Serikali katika kufanikisha kuanza kutumika kwa mfumo huo ambao unakwenda kuwa mkombozi kwa akina mama pamoja na watoto wachanga.
Aidha Dkt.Nawanda amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa Madereva wote watakaokuwa katika mfumo huo malipo yao yafanyike ndani ya masaa 24 ili kuleta ari kwa madereva hao kufanya kazi kwa weledi na kujituma katika kusaidia Jamii.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi Prisca Kayombo awali akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Dkt Nawanda amemshukuru Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa katika Sekta ya Afya.
Mratibu wa Mafunzo ya Mfumo wa M-Mama Bi.Sara William ameeleza kuwa hadi kufikia hivi sasa mafunzo kwa wauguzi 24 pamoja na madereva Jamii zaidi ya 82 wametambuliwa na kupatiwa mafunzo kwa ajili ya kuanza matumizi ya mfumo huo ambapo jumla ya vituo 282 vyA kutolea huduma za Afya vimeunganishwa kwa ajili ya kuanza kutoa huduma.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa