• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
OFISI YA MKUU WA MKOA WA SIMIYU
OFISI YA MKUU WA MKOA WA SIMIYU

.JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA .OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA OFISI YA MKUU WA MKOA WA SIMIYU

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Idara na vitengo
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA)
      • Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
  • Sekta ya Afya
    • Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
    • Huduma za Afya Mkoa
  • Sekta ya Elimu
  • Sekta ya Kilimo
    • Sekta ya Mifugo
    • Sekta ya Uvuvi
    • Sekta ya Maliasili na Mazingira
    • Sekta ya Ushirika
  • Sekta Utalii
  • Kituo cha Habari

RC SIMIYU AKAGUA UJENZI KITUO CHA KUPOOZEA UMEME BARIADI,UJENZI MRADI WA KUSAFIRISHA UMEME KV 220 SHINYANGA(IBADAKULI) -SIMIYU (BARIADI) KM 110.

Posted on: October 25th, 2023

AAGIZA WAKANDARASI KUKAMILISHA MRADI KWA WAKATI.


WANANCHI KUONDOKANA NA ADHA YA KUKATIKA KWA UMEME SIMIYU.



Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt Yahaya Nawanda amewaagiza wakandarasi wanaotekeleza mradi wa Njia kuu ya kusafirisha umeme ya Msongo wa KV 220  Shinyanga(Ibadakuli)  hadi Simiyu (Bariadi), pamoja na ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha Simiyu kukamilisha mradi huo haraka ili Wananchi waweze kuondokana na adha  ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.


Dkt.Nawanda ametoa maagizo hayo 25 Oktoba 2023 katika ziara yake katika Wilaya ya Maswa na Bariadi   iliyolenga  kukagua utekelezaji wa mradi huo.


"Tunataka ndani ya miezi 18 kipindi cha Mkataba mradi uwe umekamilika na utekelezaji wa mradi usiwe na mashaka mashaka na wamenihakilishia hapa kuwa kazi hii itakamilika ndani ya muda uliopangwa" alisema Mkuu wa Mkoa Mhe.Dkt Nawanda.


Aidha Mkuu wa  Mkoa Dkt Nawanda ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufikisha umeme katika vijiji 470 ndani ya  Mkoa wa Simiyu.


"Katika Nchi hii ni Mkoa wa Simiyu pekee  ambao hatumdai Mhe.Rais katika kijiji chochote na  kazi yetu tuliyo nayo ni kusafirisha umeme katika Vitongoji baada ya umeme huu kuongezewa Nguvu baada ya kukamilika mradi huu unaotekelezwa wa kusafirisha umeme kV 220"alisema Dkt.Nawanda.


Kwa upande wake Meneja wa  mradi huo Mhandisi   Adolf Kigombola amesema tayari kazi za awali zimeanza kutekelezwa na mkandarasi baada ya  TANESCO kwa kushirikiana na wadau wa mradi kufanya uhamasishaji  kwa Wananchi ili kuruhusu uanzaji wa kazi za awali wakati Serikali ikichakata malipo ya Fidia.


Aidha ameongeza kuwa TANESCO inafuatilia kwa karibu malipo ya Fidia kwa waathirika wa mradi na kwamba   Wananchi  watarajie  malipo ya fidia mapema Mwezi Novemba 2023.


Mkandarasi M/S Kalpataru Projects International Limited (KPIL)kutoka Nchini India anatekeleza ujenzi wa Njia kuu ya kusafirisha umeme ya Msongo wa KV 220  Shinyanga(Ibadakuli)  hadi Simiyu (Bariadi),huku kituo cha kupoozea umeme ujenzi wake  ukitekelezwa na M/S Sian Electric Engineering Co.LTD kutoka Nchini China.


Serikali imeelekeza kiasi cha shingi Bilioni 48 kwa ajili ya Utekelezaji wa mradi huo ulioanza utekelezaji wake 10 Machi 2023  ambapo unatarajiwa kukamika ifikapo 9 Septemba 2024.



GCO,

Simiyu RS,

25 Oktoba, 2023


Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 01, 2025
  • Fungua

Habari Mpya

  • MASHINDANO YA UMISETA NA UMITASHUMTA YAZINDULIWA KIMKOA MASWA. DC NGATUMBURA ASISITIZA NIDHAMU NA BIDII ILI KUPATA USHINDI KATIKA NGAZI YA TAIFA.

    May 30, 2025
  • SIMIYU RS WAHAMIA JENGO JIPYA LA UTAWALA NYAUMATA

    June 03, 2024
  • RC NAWANDA ARIDHISHWA NA UJENZI MRADI WA MAJI MWABUMA/MWASHATA MEATU.

    May 30, 2024
  • RC SIMIYU ARIDHISHWA NA MAENDELEO UJENZI WA MRADI WA USAMBAZAJI MAJI WA VIJIJI VYA SUNZULA, MWAMNEMA NA NGESHA WILAYANI ITILIMA,

    May 29, 2024
  • Fungua

Video

MIAKA MINNE YA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN MKOANI SIMIYU
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • TUME YA RAIS UKUSANYAJI MAONI MABORESHO YA KODI YATUA SIMIYU
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii
  • SIMIYU- RS TV

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Video

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa