• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka:Zoezi la Kuondoa Mifugo kwenye Maeneo ya Hifadhi Lifanyike kwa Weledi, Uadilifu na Haki

Posted on: August 31st, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Meatu mkoani humo, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo,Dkt. Joseph Chilongani kutekeleza kwa weledi, uadilifu na haki zoezi la kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi litakaloanza September 04, 2017.

Mtaka ametoa kauli hiyo mara baada ya viongozi wa Serikali na Chama Mkoa na Wilaya, Wataalam, wafugaji na wadau wa uhifadhi na Utalii kukutana na kujadili suala la uondoaji mifugo katika Maeneo ya Hifadhi, yakiwemo ya  Pori la Akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) Makao wilayani Meatu.

“Mkafanye zoezi hili kwa weledi mkubwa na haki, lisije likawa zoezi la kuwaonea watu, kufanya utapeli kwa kujifanya mnachukua ng’ombe kwa ajili ya kutaifisha halafu mkagawana; viongozi na wote mtakaohusika mkalisimamie kwa makini sana suala hili” alisisitiza Mtaka

Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe.Joseph Chilongani amesema baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi, wafugaji na wadau wa uhifadhi na utalii ametoa muda wa siku nne na kufikia Septemba 04 mwaka huu, wafugaji wawe wametoa mifugo katika maeneo ya hifadhi kwa hiari.

Dkt.Chilongani amebainisha kuwa Viongozi wa Wilaya ya Meatu walikutana na wafugaji katika maeneo yao na kuwatahadhalisha juu ya uingizwaji wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi, ili kuwasaidia waepuke adhabu ya kifungo na mifugo yao kutaifishwa kwa kuwa kuingiza mifugo hifadhini ni makosa kwa mujibu wa sheria.

“Maandalizi yote yako tayari, timu za kutekeleza zoezi hili zote zipo, nitoe muda wa siku hizi zilizobaki ili kufikia Jumatatu ya tarehe 04 zoezi la kuondoa mifugo kwenye Pori la Akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na WMA ya Makao lianze, tulishawapa wafugaji muda wa kutosha tulipokuwa tukipita kwenye vijiji kuzungumza nao juu ya madhara ya  kuingiza mifugo hifadhini” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa Pori la Akiba la Maswa Lasato Masinde amezitaja baadhi ya changamoto za kuingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi kuwa ni ushindani wa malisho na maji kati ya wanyamapori na wafugwao,ongezeko la ujangili, kuuwawa kwa wanyamapori hasa walao nyama, magonjwa na mmonyoko wa udongo kutokana na wafugaji kukata miti.

Aidha, Masinde amefafanua kuwa suala la uingizwaji wa mifugo katika hifadhi linachangiwa pia na baadhi ya viongozi wa vijiji wasiokuwa waadilifu ambao hupokea fedha kwa wafugaji na kuwaruhusu kuingiza mifugo yao, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Meatu kuwachukulia hatua stahiki wale wote watakaobainika kujihusisha na uhalifu huo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wafugaji kupima maeneo yao wanayomiliki na kuyawekea miundombinu ya mifugo kama vile visima vya maji na mabwawa, majosho na mashamba ya malisho ili waweze kufuga kisasa na kuondokana na adha ya kuhangaika kutafuta maji na malisho.

Katika kikao hicho wafugaji kwa pamoja wamekubali kutoa mifugo katika maeneo ya  hifadhi na kukubaliana na ushauri wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wa kupima maeneo yao na kuweka miundombinu, hivyo wameomba watalaam wa Ardhi na Mifugo waweze kuwasaidia namna wanavyoweza kutumia maeneo yao kufuga kisasa.

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani humo.

Baadhi ya viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.

Meneja wa Pori la Akiba la Maswa, Lusato Masinde akiwasilisha taarifa yake kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.

Katibu wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanayamapori ya Makao, Robert Simon akiwasilisha taarifa yake kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa