• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka:Walimu wa Kike Wasaidieni Wanafunzi wa Kike Kupata Elimu ya Kujitambua

Posted on: April 19th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa  wito kwa walimu wote wa kike mkoani humo kuwasaidia wanafunzi wa kike katika elimu ya kujitambua ili iwasaidie kuepukana na vishawishi vinavyoweza kupekelekea mimba za utotoni.

Mtaka ameyasema hayo jana katika Kongamano la Elimu ya Masuala ya Jinsia kwa Walimu na Wanafunzi wa Kike wa baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari za Makao Makuu, kilichofanyika katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi.

Amesema si masuala yote ya yanayohusu maisha yamewekwa katika mitaala, hivyo walimu wanapaswa kusimama katika nafasi zao kama wazazi ili kile wanachotamani kuwafundisha watoto wao au ndugu zao kwa lengo la kuwalinda na tabia zisizofaa, wakifanye pia kwa wanafunzi wao wa kike ili wawasaidie wasiharibike.

Ameongeza kuwa Viongozi  na Watendaji mbalimbali wa Serikali Mkoani humo wanatamani wanafunzi wote wa kike wanaoanza darasa la kwanza na kidato cha kwanza wamalize masomo na kufikia ndoto zao pasipo vikwazo vyovyote ikiwemo mimba za utotoni.

“Tungehitaji kuona wanafunzi wa kike wa mkoa wetu wanajitambua, tusingehitaji kuwa na wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakakatisha masomo yao na ndoto zao, natamani watoto wa kike wa Simiyu suala la elimu liwe Kipaumbele chao cha kwanza” alisema Mtaka

“Msaada wa kwanza wa watoto wetu wa kike ni walimu wetu wa kike, mwalimu anayewasimamia vizuri watoto wa kike  na kuwasaidia wasiharibike hata watoto wake nyumbani hawawezi kuharibika, ‘uki-ignore’ (ukipuuza) kwamba mwanafunzi hakuhusu kesho utakuta mwanao ndiye anayeharibikiwa” alisisitiza.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa amesema ipo haja na hoja kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike kwa shule zote za Sekondari za Kata ili watoto wa kike wasipange wala kutembea mwendo mrefu.

Kwa upande wake Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Mary Mrio amesema walimu wa kike wakiwasaidia na kuwa marafiki kwa watoto wa kike ni rahisi watoto kuwaeleza matatizo yanayowakabili na akawataka wanafunzi kuwa wawazi kwa walimu wao wa kike ili wasaidiwe

Naye Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF kupitia Mradi wa UZAZI UZIMA ametoa wito kwa watoto wa kike mkoani Simiyu kutokubali kutumiwa kama mitaji na wazazi wao kwa kukatishwa masomo na kuozeshwa mapema,  ili kukabiliana na  changamoto ya mimba za utotoni  katika kufikia ndoto zao.

Katika hatua nyingine wanafunzi wa kike wameiomba Serikali kuona namna ya kuwashirikisha wazazi na walezi wao katika makongamano ambayo yanatumika kutoa elimu ya masuala ya jinsia ili nao wawe na uelewa juu ya masuala hayo na kujua namna ya kuwasaidia watoto wao.

“Kwenye makongamano kama haya ingekuwa vizuri tukiwahusisha baadhi ya wazazi ili nao wapate elimu kama hii tunayopata sisi, maana sisi watoto wa kike kuna wakati unaweza  ukawa unaumwa  ila ukimweleza mzazi anasema hutaki kufanya kazi” Florencia Ndakama mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Shule ya Sekondari Bariadi

Akitoa taarifa juu ya ushiriki wa wanafunzi na walimu wa kike katika kongamano hilo, Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory amesema jumla ya walimu 228 na wanafunzi 1506 kutoka katika baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi wameshiriki.

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUNGUA HAPA:https://simiyuregion.blogspot.com/2018/04/rc-mtaka-walimu-wa-kike-wasaidieni.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa