• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka: Nanenane Ilenge Kutatua Tatizo la Njaa na Kuwainua Wananchi Kiuchumi

Posted on: August 9th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yalenge kuwashindanisha washiriki katika vigezo vinavyolenga kutatua tatizo la njaa na kuwainua wananchi kiuchumi badala ya kuwashindanisha kwa ujenzi wa mabanda.

Mtaka ameyasema hayo wakati akihitimisha maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa yaliyofanyika katika Uwanja wa Nyamhongolo wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.

Amesema Halmashauri zimekuwa zikishindanishwa na kupata tuzo na vyeti kwa kuwa na mabanda mazuri , kutembelewa na watu wengi na vigezo vingine vinavyowekwa kutathmini wakati wa maonesho, lakini wananchi katika baadhi ya maeneo hayo wanapata tatizo la njaa.

Ameongeza kuwa ipo haja kwa viongozi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ina uhakika wa maji ya Ziwa Victoria kuweka dhamira ya kuondokana na aibu ya kuomba chakula cha msaada ili kuisaidia Serikali.

“ Ni vizuri tujiulize sana sisi viongozi wa Kanda ya Ziwa tunaokuja kwenye maonesho ya Nanenane; ni  kwa nini Mhe.Rais asiombwe chakula maeneo yasiyo na maji ya uhakika, aombwe chakula na watu wenye maji ya uhakika, ipo haja ya kuweka dhamira ya dhati  kuondokana na aibu hii” alisema Mtaka.

Aidha Mtaka amesema ili kufanya mapinduzi katika kilimo Wataalam wa Kilimo wanapaswa kuwasaidia wakulima kuondokana na kilimo cha mazoea ili waweze kulima kilimo cha kisasa chenye tija.

Sanjali na hilo Mtaka ametoa wito kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo kuwasaidia wananchi kupata mbegu bora, mbolea na zana bora za kilimo yakiwemo matrekta ili waweze kutoka kwenye kilimo cha utamaduni(mazoea) kwenda kwenye kilimo cha kisasa chenye tija.

Mkuu huyo wa Mkoa pia ametoa rai kwa Wataalam wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoka Maofisini na kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kupata elimu ya ugani ili wafanye shughuli zao kwa tija na weledi.

“Watu wa Wizara tokeni huko wizarani njooni muwafundishe watu wetu ugani...tunakwazwa sana na ninyi watu wa Wizara hasa mnapoona ni jambo jepesi kutoa maagizo kwa wakuu wa wilaya wasimamie Kilimo wakati ninyi mnajua mnaleta mbegu zisizo na kiwango,madawa mnayoleta yana changamoto ya kuwa feki” amesema Mtaka.

Ameongeza kuwa Viongozi wa kanda ya ziwa wanaomba Wizara ya Kilimo kuja na majawabu ya kudumu ya changamoto za uzalishaji wa zao la pamba hususani upatikanaji wa mbegu bora, madawa pamoja na bei ya kuuzia pamba itakayowasaidia wakulima wa pamba.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Tathmini ya Maonesho ya Nanenane, Mathayo Masele aliitangaza Halmashauri ya Wilaya ya Busega kutoka Simiyu kuwa  Halmashauri ya kwanza kati ya Halmashauri za Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kwa kutimiza vigezo vilivyotumika kushindanisha ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Kauli Mbiu ya maonesho.

Akizungumzia ushindi huo Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya ya Busega, Ndg.Juma Chacha amesema Halmashauri hiyo ilitimiza vigezo vyote vya ushindani kwa asilimia 100 , ambapo ilikuwa na vitalu vya mfano kwa mazao ya chakula na biashara,mabanda ya mifugo mbalimbali, ufugaji wa samaki kwa ajili ya elimu kwa wakulima, wafugaji na wavuvi namna ya kuongeza thamani.

Naye Emmanuel Mgeta mkulima kutoka Busega aliyekuwa mshindi wa tatu kati ya wakulima wa mikoa ya kanda ya ziwa walioshindanishwa amesema maonesho ya Nanenane mwaka 2017 yamemsaidia kujifunza na kumpa hamasa ya kufanya vizuri katika uzalishaji na umuhimu wa kuyaongezea thamani mazao.

Kauli Mbiu ya Nane nane mwaka 2017 ni “ZALISHA KWA TIJA MAZAO YA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI ILI KUFIKIA UCHUMI WA KATI” ambapo  Mikoa ya Kanda ya Ziwa Simiyu, Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga na Kagera imeadhimisha katika Uwanja wa Nyamhongo Ilemela jijini Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Halmashauri ya wilaya ya Busega,Juma Chacha zawadi ya kombe na cheti baada ya Halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza miongoni mwa Halmashauri za Mikoa ya kanda ya Ziwa katika Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (katikati) akipata maelezo kutoka kwa watalaam wa Kilimo kuhusu zao la dengu mara baada ya kutembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Busega na kuona vitalu vya baadhi ya mazao ya Kilimo na biashara, kwenye Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa