• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Azindua Kambi ya Kitaaluma kwa Kidato Cha Sita Simiyu, Aagiza Taa Zisizimwe Wasome

Posted on: April 4th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amezindua rasmi  kambi ya kitaaluma kwa Wanafunzi wa  Kidato cha sita kwa mwaka 2019 yenye wanafunzi 1166 na kuagiza taa zisizimwe usiku ili wanafunzi waweze kupata nafasi ya kujisomea zaidi.

Mtaka ametoa agizo hilo , wakati akizindua kambi hiyo kwa wanafunzi 1166 wa kidato cha sita na walimu mahiri 34 kutoka shule 12 za mkoa wa Simiyu,  inayofanyika katika shule ya sekondari ya  wasichana ya Maswa.

Amesema ili mkoa wa SIMIYU uweze kushindana kiuchumi unapaswa kufanya mageuzi makubwa ya kielimu, hivyo elimu ni kiupaumbele cha mkoa ambapo ameagiza katika kipindi chote cha kambi wanafunzi waruhusiwe kusoma  bila kuzimiwa taa darasani.

Katika hatua nyingine Mtaka amewahakikishia wanafunzi na walimu upatikanaji wa mahitaji yote muhimu wawapo kambini, ikiwa ni pamoja na ulinzi na usalama, upatikanaji wa chakula, maji, umeme, mahitaji mengine na kueleza kuwa tayari viti vipatavyo 1000 vimeshanunuliwa kwa ajili ya kambi hiyo.

Aidha, ameahidi kutoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi, walimu na shule itakayofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha Sita mwaka 2019 “Ofisi yangu itatoa zawadi ya shilingi milioni tatu kwa mwanafunzi atakayepata ‘division one ya point tatu’ atakayepata ‘division one ya point 4 na 5’ atapata shilingi laki tano; shule itakayokuwa katika kumi bora Kitaifa itapata shilingi milioni tano” alisema.

Kuhusu walimu watakaofanya vizuri katika masomo yao, Mtaka amesema mwalimu atapata zawadi ya shilingi elfu 50 kwa kila alama A itakayopatikana kwenye somo lake, huku akiahidi pia kutoa shilingi milioni 12 kwa ajili ya posho ya walimu walio kambini.

Kwa upande wao  Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju na Mwenyekiti wa wakuu wa shule mkoa wa Simiyu, Mwl. Amede Ndonje wamekiri kuwa kambi za kitaaluma zimechangia kuongeza ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita kutoka nafasi ya 26 mwaka 2017 hadi nafasi ya 10 mwaka 2018 na kwa kidato cha nne kutoka nafasi ya 11 mwaka 2017, hadi kufikia nafasi ya tisa mwaka 2018.

Baadhi ya walimu mahiri na wanafunzi wa Kidato cha Sita wametoa maoni yao kuhusu kambi “Tuna malengo ya kufanya vizuri zaidi ya mwaka jana, kambi ya mwaka jana ilikuwa kwa siku chache tu sisi tumepewa siku 28 nina uhakikika tutazitumia vizuri na tutahakikisha mkoa wetu unakuwa wa kwanza” MkimaWarento kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa

“ Kuanzisha kambi za kitaaluma ni wazo zuri na  napenda kuwahakikishia kuwa fedha zenu mlizowekeza hapa kambini si bure, tunawaahidi kuwa hatutawaangusha sisi tumejipanga kufanya mapinduzi ya kitaaluma na tutakuwa nambari moja mwaka huu” alisema  Kasto Nyakarungu mwanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Binza.

“Nikiwa miongoni mwa walimu wawezeshaji katika kambi hii ya Kitaaluma niwahakikishie kuwa tumejipanga ipasavyo kuhakikisha mkoa wetu unaingia katika tatu bora na matarajio yetu ni kuwa nafasi ya kwanza” alisema Mwalimu Mary Kavishe anayefundisha somo la Kiswahili.

Katika uzinduzi huo wa kambi za kitaaluma wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Chama na Serikali pamoja na watumishi wa Umma wameahidi kuchangia vyakula ambavyo ni mchele zaidi ya tani mbili, maharage kilo 200, ng’ombe wawili na fedha taslimu ili kufanikisha kambi hiyo kufanyika vizuri.

Wanafunzi wa Kidato cha Sita wako kambini kuanzia tarehe Mosi Aprili, 2019 na wanatarajia kukaa kambini kwa takribani siku 28 na baadaye kutawanyika kwenda kwenye shule zao kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya Mtihani wa Taifa utakaoanza Mei 06, 2019.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/04/rc-mtaka-azindua-kambi-ya-kitaaluma-kwa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa