• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka awataka Wafanyakazi Mkoani Simiyu Kuchangamkia Fursa ili Kujiimarisha Kiuchumi

Posted on: May 1st, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewataka wafanyakazi mkoani humo kuchangamkia fursa ya viwanja katika maeneo ambayo uwekezaji mkubwa utafanyika ili waweze kujenga nyumba na majengo mengine ya biashara ambayo yatawawezesha kujiongezea kipato cha ziada.

Mtaka ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa Mkoa wa Simiyu katika Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa wilayani Itilima.

“Mwaka huu tutakuwa wenyeji wa NaneNane Kitaifa, karibu na eneo la Nanenane tunatoa eneo kwa ajili ya kujenga Chuo cha Mipango kajengeni hosteli wanafunzi wapange; tunajenga kiwanda cha vifaa Tiba Dutwa jengeni nyumba watumishi wakapange, tunajenga VETA pale Bunamhala jengeni vyumba vya biashara watu waje wapange,  Simiyu ni mahali penye fursa nyingi” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema mkoa wa Simiyu ni Mkoa wenye agenda ya maendeleo hivyo akawataka wafanyakazi, viongozi na wananchi kujiepusha kuwa watu wa matukio badala yake wajikite katika agenda ya maendeleo ya Mkoa huo.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi Katibu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu(TALGWU) Wandiba Kongoro ameomba Serikali izifanyie kazi changamoto mbalimbali za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na madeni hususani ya uhamisho, likizo na matibabu, utararibu wa upandishaji wa madaraja, baadhi ya waajiri kutoitisha mabaraza ya wafanyakazi na baadhi ya waajiri kutowapa watumishi hodari zawadi zao.

Kongoro amesema changamoto nyingine ni Michango ya wafanyakazi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutolipwa kwa wakati hasa kwa watumishi wanaolipwa kwa kutumia Makusanyo ya ndani na akawaomba waajiri kulishughulikia hili katika kipindi hiki cha mpito kabla mifuko haijaunganishwa ili kuepusha adha kwa watumishi watakapostaafu.

Nao watumishi na wananchi walikuwa na maoni mbalimbali kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Kimkoa ambayo yamefanyika kwa mara ya sita sasa tangu kuanzishwa kwa Mkoa wa Simiyu mwaka 2012

“Wana Itilima tumeipokea Mei Mosi kwa furaha sana kama mnavyoona mwitikio wa wananchi na wafanyakazi ni mkubwa, mpangilio wa matukio uko vizuri, nimevutiwa na utaratibu wa kuwasoma wafanyakazi hodari mbele ya wenzao na kuwapa zawadi, hii itawafanya wafanyakazi wengine kuwa na bidii ili nao wapate ” alisema Peter Karume Shimo mwananchi kutoka Itilima.

“Siku hii tumeipokea vizuri na Mkuu wetu wa Mkoa ametuambia mambo mazuri ya kutufanya tuweze kujiimarisha kiuchumi kama watumishi na vile vile kufanya kazi zetu kwa weledi, binafsi nawashauri wafanyakazi wenzangu tufanye vile tunavyoelekezwa na viongozi wetu” alisema Mwamba Isaya Venance Mwalimu wa Shule ya Msingi Munze wilayani Itilima,

Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi mwaka 2018 yamefanyika chini ya Kaulimbiu inayosema “KUUNGANISHWA KWA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII, KULENGE KUBORESHA MAFAO YA WAFANYAKAZI”

MWISHO.


kUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU NAMNA MEIMOSI ILIVYOADHIMSHWA SIMIYU FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/05/rc-mtaka-awataka-wafanyakazi-mkoani.html


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa