• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Awataka Viongozi wa Serikali Simiyu Kuisaidia, Kuilea Sekta Binafsi

Posted on: June 23rd, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewataka viongozi wa Serikali mkoani Simiyu kuisaidia na kuilea Sekta Binafsi ili iendelee kukua na wahakikishe kuwa maamuzi wanayofanya hayawi vikwazo  katika mazingira ya biashara na uwekezaji.

 

Mtaka ameyasema hayo wakati akifungua Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu ambayo imefanyika mjini Bariadi.

Amesema viongozi wa Serikali mkoani humo wanapofanya maamuzi katika biashara za watu ni lazima wawe na nia ya dhati ya kuona sekta binafsi inakuwa, ili maamuzi ya viongozi hao yasiwe vikwazo kwa ukuaji wa Sekta binafsi na mazingira ya biashara na uwekezaji.

“Sekta binafsi ni lazima ilelewe anaeilea ni Serikali, Sekta binafsi ni lazima ilindwe anayeilinda ni Serikali,Sekta binafsi ni lazima isimamiwe anayeisimamia ni Serikali na Serikali inaisimamia kwa maana ya kuilea ili ifanye vizuri” alisema Mtaka.

Aidha, ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya mkoani Simiyu kuendeleza utaratibu wa kukutana na wafanyabishara ili kupata nafasi ya kujadiliana juu ya fursa mbalimbali za uwekezaji na namna ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, huku akisisitiza pia kuendelea kufanyika kwa mabaraza ya biashara ya wilaya.

Katibu wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA) Mkoa wa Simiyu, Bi. Christina Matulanya amesema ili kuboresha mazingira ya biashara Serikali inapaswa kuendelea kuvutia wawekezaji  na kusimamia sheria, sera na kanuni zisipindishwe, huku akiupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuandaa mwongozo wa uwekezaji.

Katika hatua nyingine Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Charles Mkumbwa  ametoa wito kwa wafanyabiashara kuwa wazalendo, kutoa risiti ipasavyo, kufuata sheria za kodi na akaahidi kuwapa ushirikiano wafanyabiashara kila wanapohitaji.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule ya biashara,  Khalidi Swabiri ambaye alikuwa mwezeshaji wa warsha hii amesema ni vema mabaraza ya biashara ya wilaya yakafanyika ili wafanyabiashara wapate muda wa kukutana na viongozi wa Serikali, sekta binafsi kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika mazingira ya biashara na uwekezaji na ufumbuzi wake.

Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA), Dkt. Meshack Kulwa  amesema pamoja na kuomba mabaraza ya biashara ya wilaya yafanye kazi, ameomba  TCCIA mkoani Simiyu itafute viongozi watakaofanya kazi kwa kujituma ili TCCIA Simiyu iweze kuwa imara.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/06/rc-mtaka-awataka-viongozi-wa-serikali.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa