Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amekabidhi pikipiki za maafisa Ugani na Gari la Idara ya Kilimo wilayani Itilima na kusisitiza kuwa vyombo hivyo vitumike kwa ajili ya kuwafikia wananchi ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao hususani zao la pamba.
Vyombo hivyo ambavyo awali vilikuwa vimeegeshwa vimefanyiwa matengenezo kwa gharama za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka, aliyoyatoa wakati wa ziara yake aliyofanya katika Halmashauri zote Mkoani humo kwa lengo la kuhimiza kilimo.
Mtaka amesema zao la pamba linachangia mapato ya Halmashauri kwa kiasi kikubwa Mkoani humo hivyo Wakurugenzi wanapaswa kuhakikisha vyombo vya usafiri vinafanya kazi muda wote wa msimu ili wataalam waweze kuwafikia wakulima(wananchi) na kuwasaidia kuzalisha kwa tija.
“ Mwaka 2016/2017 Itilima ilipata milioni 500 kutokana na pamba lakini Idara ya Kilimo iliyosababisha Pamba kuleta fedha hizo haikutengewa fedha kwenye bajeti, haikuwa na gari wala pikipiki” amesema Mtaka.
“ Wakati wa kilimo hakuna magari kwa ajili ya kuwafikia wakulima, wakati wa kukusanya ushuru magari yote yanakuwa mazima na yanawekwa mafuta ili kufuatilia ushuru, maelekezo yangu kwa Halmashauri zote ni kwamba wakati wote wa msimu wananchi kuanzia wanapoandaa mashamba ni lazima pikipiki na magari yafanye kazi kwenye Idara ya Kilimo ” amesititiza Mtaka.
Wakipokea pikipiki na gari la Idara Maafisa Ugani hao wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanawafikia wakulima wote walio katika maeneo yao, ili kupitia utaalamu wao waweze kuwasaidia kuongeza uzalishaji, ambapo wamekusudia kuongeza uzalishaji wa pamba kwa mwaka 2017/2018 kutoka kilo 650 hadi 1200 kwa ekari.
Mkoa wa SIMIYU ni mkoa unaozalisha pamba kwa wingi ambapo unazalishaji asilimia 60 ya pamba yote hapa nchini
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa