• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Awahimiza Wananchi Simiyu Kuwapeleka Watoto Kupata Chanjo ya Surua-Rubella

Posted on: October 18th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amezindua zoezi la utoaji wa chanjo ya Surua-Rubella kwa watoto wenye umri kuanzia miezi tisa hadi miezi 59 (chini ya miaka mitano) na kuwahimiza wananchi kuwapeleka watoto kupata chanjo hiyo inayotolewa bila malipo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na vituo vya muda  vilivyotengwa vipatavyo 405, ili kuwakinga watoto hao na maradhi.

Akizungumza na wananchi walioshiriki katika uzinduzi wa zoezi hilo Oktoba 17, 2017 katika Kituo cha Afya cha Muungano Mjini Bariadi,  Mtaka amesema ni vema wananchi hao watumie siku zilizotengwa kutoa chanjo hiyo kuanzia Oktoba 17-21, 2019 kuwapeleka watoto kwenye chanjo  na wawe mabalozi wema kwa wenzao.

“Madhara ya Surua ni pamoja na masikio ya mtoto kutoa usaha utakaosababisha mtoto kuwa kiziwi, vidonda vya macho vinavyoweza kusababisha upofu, utapiamlo, kuvimba ubongo, udumavu wa akili na kifo; mliokuja leo mkawe mabalozi wema kwa wenzenu wawalete watoto chanjo ili watoto wakingwe dhidi ya haya magonjwa,” alisema Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka  amewataka wananchi kutumia vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo kwenye maeneo yao kupata huduma za matibabu ili waweze kupata tiba sahihi kwa wakati sahihi badala ya kwenda kwa waganga kupiga ramli.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange amesema watoto takribani 420,000 wanatarajiwa kupata chanjo ya Surua-Rubella, ambapo chanjo hiyo itakuwa ikitolea kuanzia saa moja asubuhi hadi saa 12 jioni.

Kwa upande wake mmoja wa wazazi waliowapeleka watoto wao kwenye Bw. Hamza Adam amesema ni vema kila mzazi mwenye mtoto wa umri chini ya miaka mitano ampeleke akapate chanjo ya Surua-Rubella, ili wawakinge na maradhi hayo na kuwaomba wasiwapeleke kwa waganga wa jadi wanapokuwa wagonjwa.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Benki Mjini Bariadi, Consolata Cosmas  amesema wenyeviti wa Mitaa na Vijiji mkoani Simiyu wameshiriki kikamilifu katika kuhamasisha waananchi kupeleka watoto kupata chanjo, hivyo imani yao ni kwamba zoezi hilo litafanikiwa kwa kuhakikisha watoto wote waliopangwa kupewa chanjo wanapewa na lengo linafikiwa.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/10/rc-mtaka-awahimiza-wananchi-simiyu.html

 

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa