• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka atoa Wito kwa Walimu kuepuka vitendo vinavyoharibu Haiba na Heshima ya Ualimu

Posted on: November 29th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa walimu kuendelea kuwa walezi wa wanafunzi wao na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoharibu haiba na heshima ya ualimu, ili waweze kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili kwao  na  kwa wanafunzi wanaowafundisha.

Mtaka ameyasema hayo Novemba 28, 2018 katika mahafali ya 26 ya kidato cha nne shule ya sekondari Mwembeni (ambayo alisoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne mwaka 1997-mwaka 2000), iliyopo Mjini Musoma ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Amesema katika baadhi ya maeneo baadhi ya walimu wamekuwa wakifanya mambo ambayo yanaharibu heshima na haiba ya ualimu jambo ambalo linapelekea wazazi kutowaamini walimu na kuogopa kuwapeleka watoto wao katika shule hizo.

" Naishukuru sana bodi ya shule na walimu wa Mwembeni kwa kuendelea kuhakikisha walimu wetu wanalinda heshima na haiba ya ualimu na wazazi wameendelea kuiamini shule kwa kuleta watoto wao, kwa sababu hakuna matukio yanayohatarisha uwepo wa watoto wao shuleni na masuala la elimu, maadili na nidhamu kwenye shule hii kama Taasisi yameendelea kuimarishwa" alisema.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wazazi, walezi na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wanafunzi waliosoma katika shule ya Mwembeni miaka ya nyuma kuchangia katika ujenzi wa shule(vyumba vya madarasa) ili kupanua wigo kwa wanafunzi kuanza kusoma masomo ya sayansi, ikizingatiwa kuwa katika dunia ya sasa ni ya ushindani wa sayansi na teknolojia.

"Dunia tunayoiendea sasa ni ya ushindani wa sayansi na teknolojia na kama shule imejielekeza kwenye masomo ya sayansi ni jambo la kuungwa mkono; niwaalike wenzangu wote tuliosoma katika shule ya sekondari Mwembeni kuona haja ya kurejesha kwenye shule katika kile tulichopata katika shughuli zetu za kimaisha, tukirejeshe tujenge shule yetu ili iendelee kuwa kwenye ushindani mkubwa na kuwa miongoni mwa shule bora mkoani Mara" alisisitiza Mtaka.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwembeni, Bro.Erasmus Marando amewaomba wadau wasaidie kujenga vyumba zaidi vya madarasa, shule hiyo ianze kutoa masomo ya mchepuo wa sayansi, ili kuwaanda wataalam watakaoenda sambamba na sera ya Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Viwanda.

Naye Mwalimu Anselm Mnibhi ambaye amemfundisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Shule ya Sekondari ya Mwembeni mwaka 1997 hadi mwaka 2000, amemshukuru kwa kukumbuka shule aliyosoma na kuonesha nia ya kusaidia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na kubainisha kuwa hakuna mwanafunzi yeyote aliyesoma hapo zamani aliyeonesha nia na dhamira hiyo na akawaomba wote waliosoma shuleni hapo kujitoa kujenga shule yao.

Kwa upande wake mhitimu wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mwembeni, Sharon Buganda ametoa wito kwa wanafunzi waliobaki kuondokana na dhana ya kuogopa kusoma masomo ya sayansi wakiamini kuwa ni magumu, badala yake wasome masomo hayo ili waweze kuwa wataalam wajao katika maeneo mbalimbali ikiwemo viwanda ambavyo ni sera ya Serikali ya Awamu ya tano.

Katika mahafali hayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka aliahidi kuchangia shilingi milioni tano na kuhamasisha wenzake aliosoma nao shuleni hapo Mwembeni kuchangia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa vitakavyotumika na wanafunzi wa mchepuo wa sayansi, kutoa zawadi ya shilingi milioni moja (kwa mwanafunzi wa kiume) na shilingi milioni moja na laki tano(kwa mwanafunzi wa kike) atakayekuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa  katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2018.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/11/rc-mtaka-atoa-wito-kwa-walimu-kuepuka.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa