Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Jambo Food Produsts Company, Mhe. Salum Khamis na wadhamini wengine waliojitokeza kudhamini Tamasha la Simiyu Jambo Festival kuliendeleza tamasha hilo kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa mkoa wa Simiyu kuendeleza vipaji vyao katika sanaa, utamaduni na michezo.
Mtaka ameyasema hayo wakati akifunga Tamasha hilo Juni 30, 2019 Mjini Bariadi ambalo lilihusisha mashindano ya ngoma za asili (Mbina Wagika na Wagalu), mashindano ya baiskeli kwa wanawake na wanaume, mashindano ya mdahalo kwa wanafunzi wa shule za sekondari na mbio fupi(fun run).
“ Namshukuru sana Mkurugenzi wa Jambo Food Products Company Salum Khamis ambaye amekuwa mdhamini kwa miaka mitatu mfululizo kwenye tamasha hili, nimuombe yeye na kampuni yake waendelee kuunga mkono juhudi hizi kwenye eneo la michezo na burudani, sisi ni viongozi leo tupo kesho hatupo, ni vizuri jambo hili ambalo tumelianzisha kampuni yake iendelee kulimiliki kama makampuni mengine ya vinywaji yanavyofanya” alisema ikaliendeleza.
Akizungumzia Kauli Mbiu ya Simiyu Jambo Festival: WEZESHA MTOTO WA KIKE ATIMIZE NDOTO ZAKE, INAWEZEKANA KUZUIA MIMBA KATIKA UMRI MDOGO; Mtaka amesema ni vema watoto wa kike walindwe ili waweze kuepuka mimba za utotoni na kufikia ndoto zao.
Akizungumza na wananchi wakati wa Tamasha la Simiyu Festival Mdhamini Mkuu wa Tamasha hilo Mkurugenzi wa Jambo Food Products Company Salum Khamis amesema Kampuni yake itaendelea kudhamni tukio hilo na kuahidi kuendeleza tamasha hilo.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) mkoani Simiyu, Dkt. Amir Batenga amesema moja ya ahadi za shirika hilo ni kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao hivyo kupitia kauli mbiu ya tamasha hilo shirika hilo lilifikisha ujumbe kwa vijana na wanaamini kila kijana anaweza kutimiza ndoto zake.
Katika tamasha hilo washiriki zaidi ya 150 walishiriki mbio za baiskeli na mshindi wa kwanza kilometa 150 wanaume alijinyakulia kitita cha shilingi 1,000,000/=, kilometa 80 wanawake shilingi 700,000 na walemavu kilometa tano shilingi 500,000/=, huku ngoma za asili Wagika na Wagalu kila kikundi kilijipatia shilingi 1,000,000/=
Simiyu Jambo Festival mwaka 2019 imedhaminiwa na Jambo Food Products Company, Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani-UNFPA, NGM Gold Mine Limited, NGS Petroleum, Alliance Ginneries Limited, Busega Mazao Limited, Maswa Standard Chalk, Ms Hotel, Vetreces Company Limited na NHIF.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/07/rc-mtaka-atoa-wito-kwa-wadhamini-wa.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa