• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Atekeleza Agizo la Rais, Kuwagawia Vitambulisho Wajasiriamali Wadogo

Posted on: December 11th, 2018

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.  Anthony Mtaka ametekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo, ambapo amewakabidhi Wakuu wa Wilaya na Maafisa Biashara wa Halmashauri mkoani hapa jumla ya vitambulisho  25,000, vitakavyotolewa kwa wajasiriamali wadogo wenye mauzo pungufu ya milioni nne kwa mwaka.

Akikabidhi vitambulisho hivyo Mtaka amesema vitawasaidia wajasiriamali wadogo kutambuliwa,kuwajengea ujasiri na uthubutu  na kuwafanya kunufaika  na fursa mbalimbali huku akibainisha kuwa vitachangia pia kuwaibua wajasiriamali wapya mkoani Simiyu.

Ameongeza kuwa Simiyu imejipanga kuwafikia wajasiriamali wote wadogo kama ilivyokusudiwa na Mhe. Rais, huku akiwaonya na kuwatahadharisha wafanyabiashara wakubwa wanaotambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutojaribu kujipatia vitambulisho vya wajasiriamali wadogo kwa njia ya udanganyifu.

“Niwatahadharishe wafanyabiashara wasije wakatumia nafasi ya vitambulisho hivi vya wajasirimali wadogo, kufanya udanganyifu wowote wa wao kuvitumia vitambulisho hivyo kujitambulisha kama wafanyabiashara wadogo; huu udanganyifu hatutaupa nafasi na sisi kama Serikali tumejiandaa kuainisha kila mtu anachofanya, mahali anapokaa, historia yake ya biashara”

“Ofisi za Wakurugenzi zitatoa magari yatakayowawezesha maafisa Biashara kwenda vijijini kuwafikia wajasiamali wadogo,tunaamini walengwa wa vitambulisho hivi ni wale ambao nauli ya kule aliko na Makao Makuu ya Wilaya inaweza kuwa ndiyo fedha inayohitajika achangie kupata kitambulisho hicho,kwa hiyo kuna kadi zitabaki wilayani lakini nyingine zitapelekwa mahali walipo walengwa” alifafanua Mtaka.

Baadhi ya wakuu wa wilaya wakizungumza mara baada ya kupokea vitambulisho hivyo wamesema watahakikisha vinawafikia walengwa waliokusudiwa na hakutakuwepo na udanganyifu wowote katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo.

“Niwahakikishie wajasiriamali wadogo wote kuwa watapata vitambulisho kama Mhe Rais alivyoelekeza na nitoe wito kwao kuja kuchukua vitambulisho hivi ili asiwepo mtu yeyote wa kuwabugudhi na wafanye kazi zao kwa uhuru” Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga

“ Niwatoe hofu wajasiriamali wote wadogo kuwa kila aliye na sifa ya kupata kitambulisho hiki atapata na kwa wale wanaodhani watatumia vitambulisho hivi kukwepa kodi nichukue nafasi hii kutoa onyo kuwa hatutavumilia udanganyifu wa aina yoyote” Mkuu wa Wilaya ya Busega,Mhe. Tano Mwera.

Baadhi ya wajasiriamali Wadogo Mkoa Simiyu wameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli  kwa kutoa  vitambulisho hivyo ambavyo vitawaondolea adha mbalimbali walizokuwa wakizipata ikiwepo ya kuogopa kufanya biashar zao kutokana na   kutotambuliwa rasmi.

“ Tanamshukuru sana Rais ametupa ujasiri wa kufanya biashara zetu kwa uhuru maana kuna watu walikuwa wanaogopa kufanya biashara kwa sababu ya kuogopa kodi, kupitia vitambulisho hivi tutafanya biashara kwa uaminifu, uhuru na ujasiri na katika wilaya yetu ya Bariadi,  Tanzania ya Viwanda hasa vile vidogo itawezekana” alisema  Bahati Kaitila mjasiriamali mdogo kutoka Bariadi.

“ Nimelipokea vizuri suala la kupewa vitambulisho  kwa sababu vitatusaidia sisi wajasiriamali wadogo kupata ujasiri zaidi wa kufanya kazi zetu, tunaweza kuanza na kitu kidogo lakini baadaye tukafanya makubwa” alisema   Grace Mukali mjasiriamali mdogo kutoka wilaya ya Bariadi.

MWISHO.

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-http://simiyuregion.blogspot.com/2018/12/rc-mtaka-atekeleza-agizo-la-rais.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa