Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Itilima kuhakikisha inawalipa madiwani wake malimbikizo ya madeni kupitia fedha za makusanyo ya pamba mwaka huu ili kuondoa usumbufu ambao unaweza kujitokeza pindi watakapokuwa wamemaliza muda wao.
Mtaka ameyasema hayo Julai 02, 2019 wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza maalumu la madiwani llililokuwa na agenda moja ya kujadili hoja 39 za ukaguzi zilizoibuliwa na mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu za serikali ( CAG).
“ni vyema madeni ya waheshimiwa madiwani yakalipwa kwa wakati ni ngumu kujadili vitu vya kimaendeleo wakati wao wanadai, huwezi kushugulikia ya wengine wakati yako hayako vizuri, ikumbukwe wamebakiza muda mfupi baraza livunjwe …si vyema wakatoka madarakani huku wakiwa wanadai”alisema Mtaka na kuongeza kuwa .
“Mkurugenzi hakikisha kipaumbele kwenye makusanyo ya pamba unalipa madeni ya waheshimiwa hawa (madiwani) hakikisha unahuisha bima zao, lakini kingine hakikisha unatenga fedha kwa ajili ya uchaguzi ” aliongeza.
Awali akisoma taarifa ya ripoti ya mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG ) mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Elizabeth Gumbo alisema kwa mwaka wa fedha 2018/19 hoja zilizoibuliwa ni 39 na kuongeza kuwa hoja 24 kati ya 39 zilizoibuliwa zilitolewa mapendekezo na kuwasilishwa kwa mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu za serikali kwa ajili ya uhakiki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mhe. Daudi Nyalamu amesema madiwani wanadai zaidi ya shilingi milioni 360 huku akiongeza tayari halmashauri imaishajipanga kulipa madeni yote kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo.
Nao baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa kata ya Lugulu Robert Jongela na gertuda ngokolo diwani wa viti maalum kutoka kata ya ikindilo wamesema madeni yao ni ya muda mrefu tangu mwaka 2016 hadi 2019 hivyo kupitia kauli ya mkuu wa mkoa huo imewapa faraja na hatua hiyo imetoa tumain jipya la kupata stahiki zao,
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/07/rc-mtaka-ataka-madiwani-itilima-walipwe.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa