• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Asitisha Malipo ya shilingi Bilioni 1.9 kwa Wakandarasi Walioshindwa Kukamilisha Miradi

Posted on: February 16th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesitisha malipo ya shilingi bilioni 1.9   kwa wakandarasi watatu, ambao ni Simiyu Investiment Co. Ltd,  Nselema Associtates Co. Ltd na Great Lakes Construction Co.LTD, wanaotekeleza miradi saba ya maji wilayani MEATU ambayo imeshindwa kukamilika tangu mwaka 2014.

Agizo hilo amelitoa wilayani Meatu, mara baada ya kukagua miradi ya maji ya Lubiga, Itinje na Bukundi na kutoridhishwa na kazi iliyofanyika.

“Tunasitisha malipo yote ya wakandarasi  watatu wanatekeleza  miradi saba ya maji ndani ya Wilaya ya Meatu, malipo yafanyike baada ya Wataalam wetu wanasheria, wahandisi wa maji wa Halmashauri ya Meatu, Mhandisi wa Maji Mkoa,  Mwanasheria ya Mkoa na timu ya Mkoa kujiridhisha; ikiwa wanastahili kulipwa watalipwa ikibainika hawana sifa tunavunja mkataba” alisisitiza Mtaka.

Pamoja na kusitisha malipo hayo Mtaka amesema makampuni hayo hayataruhusiwa kufanya kazi za ukandarasi katika miradi yoyote wilayani humo.

Katika hatua nyingine Mtaka amewataka Viongozi wa Kisiasa wilayani Meatu wanaomiliki Makampuni ya Ukandarasi kuacha mara moja kuomba kazi za ujenzi wa miradi mbalimbali katika Halmashauri hiyo badala yake waombe katika Halmashauri jirani Mkoani humo ili kuepuka mgongano wa kimaslahi.

Aidha, amekemea tabia ya baadhi ya viongozi hao wa kisiasa ya kuwapigia simu watumishi wa Halmashauri kwa lengo la kuomba kazi au kudai malipo ya kazi zao na akawahadharisha kuwa endapo hawataacha tabia hii majina yao yatawekwa wazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Ndg.Fabian Manoza amesema kuwa wakandarasi hao waliochaguliwa na bodi ya zabuni na kupitishwa katika vikao vya baraza la madiwani kutekeleza miradi hiyo hawana uwezo.

 “Wakandarasi wanaotekeleza miradi hii hawana uwezo wanasubiri walipwe ndiyo kazi ifanyike, pia nikiri kuwa ni kweli kabisa miradi hii inatekelezwa na wanasiasa ndiyo maana hii Halmashauri ya Meatu kuiongoza tunapata shida sana, pale unaposimamia sheria unaitwa kwenye vikao  na kuazimiwa, lakini kama viongozi hasa tulioteuliwa tutasimamia sheria na taratibu” alisema Manoza.

Naye Afisa Ugavi ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Manunuzi Ndg. Emmanuel Marwa amesema kuwa taratibu za manunuzi hazikufuatwa katika upatikanaji wa wakandarasi hao ikiwa ni pamoja na Kampuni moja kupewa kusaini mkataba wa kazi zaidi ya moja.

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt.Joseph Chilongani, ameunga mkono agizo la Mkuu wa Mkoa la kusitisha malipo na kuangalia namna ya kuvunja mikataba  na akabainisha kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto katika utekelezaji wa sheria na maelekezo  mbalimbali kutokana na baadhi ya viongozi kuingilia utekelezaji hivyo ni vema hatua zichukuliwe.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/02/rc-simiyu-asitisha-malipo-ya-shilingi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa