• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Apiga Marufuku Watoa Mikopo Kushikilia Kadi za Benki Kama Dhamana

Posted on: February 29th, 2020

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amepiga marufuku wakopeshaji wanaowakopesha walimu,  kushikilia kadi zao za kutolea fedha benki (ATM) na vyeti vya taaluma kama dhamana ya mkopo.

Mtaka ametoa marufuku hiyo wilayani Itilima wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri katika  mitihani ya kitaifa mwaka 2019.

“Walimu jiepusheni na mikopo isiyo na ulazima, benki yenu ipo itumieni; imefika wakati  walimu wanaweka kadi zao za  ATM kama dhamana wengine wanaweka mpaka vyeti vya taaluma; hii biashara hapana, kitambulisho cha benki na vyeti ni mali mwalimu,”alisema Mtaka.

Aidha, amewapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwaeleza kuwa wana nafasi kubwa ya kuufanya mkoa kufanya vizuri  zaidi katika mitihani yote ya Kitaifa  ambapo ameeleza kuwa lengo la Mkoa ni kutoka kwenye nafasi kumi bora na kushika nafasi tatu bora kwa mitihani yote ya Kitaifa kwa shule za msingi na sekondari.

Katika hatua nyingine Mtaka ameendelea kusisitiza utekelezaji wa agizo la walimu kupewa kiupaumbele kuhudumiwa katika taasisi za Umma ili wapate muda wa kwenda kuwafundisha wanafunzi wanaowaacha shuleni wakati wanapoenda kupata huduma.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wialya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo amesema hali ya ufaulu katika Halmashauri hiyo imekuwa ikipanda kila mwaka, kutoka asilimia 56.2 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 78.52 mwaka 2019.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ametoa wito kwa walimu na wadau wengine wa elimu kutekeleza mkakati wa elimu wa mkoa kila mmoja kwa nafasi yake ili mkoa uweze kufikia lengo la kuwa miongoni mwa mikoa mitatu bora.

Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga amewapongeza walimu kwa kazi nzuri waliyofanya na kuahidi kuwa Wilaya hiyo itaendela kufanya vizuri kimkoa na Kitaifa huku akieleza  mpango wa Wilaya ya Itilima kuwa ni kuhakikisha kila shule ya sekondari wilayani humo inakuwa na bweni.

Nao walimu wa Wilaya ya Itilima wamesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa bidii huku wakiahidi kutekeleza ikakati yote inayowekwa katika ngazi ya Mkoa, wilaya mpaka ngazi ya shule ili waweze kufikia azma ya kuufikisha mkoa katika mikoa tatu bora nchini katika mitihani yote ya Kitaifa.

“Kutokana na mikakati ambayo mkoa umeweka ukiwemo wa kambi za kitaaluma na wanafunzi kupata chakula cha machana shuleni itasaidia sana kuinua ufaulu kwa shule za msingi na sekondari,” alisema mwalimu Bindi Busagala.

Shule na walimu waliofanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa wamepewa zawadi ya vyeti na fedha taslimu.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/03/rc-mtaka-apiga-marufuku-watoa-mikopo.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa