• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Apewa Tuzo na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA)

Posted on: September 6th, 2017


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amepewa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ikiwa ni alama ya kutambua mchango wake na kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.

Akikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa AWAMATA Taifa, Mwenyekiti wa AWAMATA Mkoa wa  Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo amesema Asasi hiyo imehamasika kutoa tuzo ya cheti kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa sababu ni mzalendo na amekuwa akifikiri juu ya maendeleo ya wananchi na namna mbalimbali za kuzalisha ajira kwa vijana.

Amesema Mhe.Mtaka ni moja ya viongozi wabunifu sana na kama kiongozi kijana amekuwa na maono makubwa yenye manufaa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla, ambapo amehamasisha uanzishwaji wa viwanda katika Mkoa kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” na  Kilimo cha Umwagiliaji wilayani Busega.

“Mhe.Mtaka tumeanza kumfuatilia toka akiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Wilaya ya Hai mpaka na baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, tumekaa kama asasi tukashawishika kumpa tuzo hii, kwa sababu amekuwa anafanya kazi ya kizalendo na maendeleo hasa anapoumiza kichwa kwa ajili ya kutengeneza ajira; tena kila wilaya kwenye mkoa wake ina kitu cha kufanya” alisema Golyo.

Akipokea tuzo hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameishukuru Asasi ya AWAMATA kwa kutambua mchango wa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na akabainisha kuwa imeipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Viongozi wa Mkoa huo pamoja na wadau wote wanaounga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo ya Mkoa na wananchi kwa ujumla.

Mtaka amesema viongozi wa mkoa huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wataendelea kujenga nuru ya matumaini kwa vijana ambao matarajio yao makubwa ni kuona kuwa wanapata kitu cha kufanya ili waweze kuendesha maisha yao.

Ameongeza kuwa miradi mingi inayoendelea ya Kiwanda cha Chaki, kiwanda cha kusindika maziwa na mingine inayofanywa katika ngazi ya viwanda vidogo vidogo ilianzishwa kwa sababu, mkoa unataka kujenga utamaduni kwa wananchi hususani vijana kujua kwamba wanaweza kuthubutu kwa kuanzia ngazi ya chini.

“ Pale Mkula Busega tulianza na vijana waliokuwa wanatengeneza viatu pair mbili tumewapa mtaji wa milioni 12 wameongeza uzalishaji na tumeomba Baraza la uwezeshaji wananchi Kiuchumi watawapa fedha ili wanunue mashine kubwa, pia tunajipanga kwa kilimo cha umwagiliaji; tunataka kuwa Mkoa ambao wananchi wake wana kitu cha kufanya na wanakiona kwenye vitendo badala ya kukiona kwenye hotuba nzuri.”

Katika hatua nyingine Mtaka amewaambia viongozi wa AWAMATA kuwa, pamoja na kutoa tuzo kwa viogozi kama walivyofanya kwake wanapaswa pia kuwakosoa viongozi hususani vijana bila kuwaonea (kuwakosoa katika haki) pale wanapoona hawafanyi vizuri, hii itawasaidia kuthibitisha dhamira ya Mhe.Rais ya kuwateua, maana ya kupewa uongozi katika kipindi hiki na kubeba dhamana kwa vizazi vijavyo.

Wakati huo huo ametoa wito kwa Viongozi wenzake vijana kutimiza wajibu wao, kuepuka maneno yanayowasahaulisha walikotoka wanapozungumzia maisha ya vijana wenzao na kukubali kukosolewa, ili wajengwe kuwa viongozi wazuri wa leo na vizazi vijavyo; kwa kuwa matarajio ya Rais katika kuwateua ni kuwa na kizazi endelevu kwenye uongozi wa nchi.

Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ni asasi ya Kiraia inayojishughulisha na uelimishaji wa uzalendo kwa Watanzania na kufundisha mbinu za kujitegemea ili kuondokana na umaskini pia inatoa tuzo kwa watu wanaofanya vizuri masuala mbalimbali ya kizalendo na kuwasaidia wananchi kutoka katika umaskini.  


 Kutoka kulia Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka, Katibu wa AMAWATA mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo na Afisa Uhusiano wa AWAMATA, Ndg Shushu Joel wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi tuzo ya cheti iliyotoloewa kama alama ya kutambua kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa AWAMATA na wadau wengene wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa