• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka Aongoza Wananchi Mazishi ya RC Mstaafu wa Shinyanga Brigedia Jenerali. Dkt.Balele

Posted on: May 9th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka leo Mei 09, 2019 amewaongoza mamia ya waombolezaji kutoka Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mwanza , Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, katika mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambayo yamefanyika katika eneo la Malinoni, Mtaa wa Kidinda Mjini Bariadi.

Akizungumza na waombolezaji hao kabla ya kuaga mwili wa Marehemu Dkt.Balele, Mtaka amesema mkoa wa Simiyu unatambua mchango wa Marehemu katika jitihada za kuanzisha mkoa wa Simiyu na mapinduzi makubwa aliyoyafanya katika Elimu na kuahidi kuweka alama yake katika mkoa kumuenzi.

"Uongozi wa Mkoa kwa kutambua mchango wa Marehemu Dkt.Balele katika kuanzisha mkoa huu na katika mapinduzi ya Elimu aliyoyafanya wilayani Bariadi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, tunaweka alama ya maisha yake kama kumbukumbu katika Shule ya Sekondari Majahida ambayo itabadilishwa Jina kuwa Dkt.Balele Sekondari na Barabara moja katikati ya Mji wa Bariadi itaitwa Barabara ya Dkt.Balele" alisema Mtaka.

Akisoma Wasifu wa Marehemu, Dkt.Balele Kapteni Zaharani Masimba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) amesema amelitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa zaidi ya miaka 32 na kutunikiwa medali mbalimbali, ikiwemo ya Vita, Kagera, miaka 20 ya JWTZ, Miaka 40 ya JWTZ, Utumishi wa muda mrefu na Utumishi uliotukuka.

Naye mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, Brigedia Jenerali, Robson Mboli Mwanjela amesema, licha ya Marehemu kustaafu Jeshi, alitumia vizuri taaluma yake ya Udaktari kuwasaidia watu mbalimbali na kuwataka wananchi wa Simiyu kuiga mema mengi aliyoyafanya.

"Marehemu atakumbukwa daima kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati wa utumishi wake jeshini na kwa Taifa kwa ujumla, katika vyeo na madaraka mbalimbali aliyopewa wakati wa utumishi wake na hata baada ya kustaafu" alisema Brig. Jen. Mwanjela.

Nao baadhi ya viongozi waliofanya kazi na Marehemu Dkt. Balele wamemuelezea kuwa alikuwa mwaminifu, mchapakazi, hodari na mwenye Upendo huku wakitoa wito kwa wananchi Mkoani Simiyu na hapa nchini kwa ujumla kuyaenzi mema yake.

"Dkt.Balele alikuwa kiongozi halisi maana alitumia uwezo na ushawishi wake kuwafanya watu wake wawe kama anavyotamani wawe, alipenda sana Elimu alitaka watu wasome na pengine hata zaidi yake, ndiye aliyehamasisha Wafanyabiashara kujenga Biashara Sekondari hapa BARIADI, naomba wana Simiyu tumuenzi kwa kuwekeza katika elimu" alisema Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Change

"Marehemu Dkt.Balele alikuwa mdau mkubwa wa Elimu katika kipindi chake alifanikiwa kuanzisha shule za Sekondari 44 Wilaya ya Bariadi na Itilima ambayo pia kipindi hicho ilikuwa sehemu ya Bariadi, lakini pia wakati wa mpango wa kuugawa mkoa wa Shinyanga alikuwa na mchango mkubwa wa kuanzisha mkoa wa Simiyu na makao makuu kuwa Bariadi, naomba tuendelee kuenzi mema yake" Baraka Konisaga, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mstaafu.

Marehemu Dkt.Balele ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mwaka 2006 hadi mwaka 2011 alizaliwa Desemba 28, 1948 katika Kijiji Cha Kasoli wilayani Bariadi na alipatwa na mauti Mei 02, 2019 katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/05/rc-mtaka-aongoza-wananchi-mazishi-ya-rc.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa