Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amemwagiza Mkandarasi wa Kampuni ya China ya CCECC inayotekeleza mradi wa maji LAMADI kuukamilisha kabla ya mwezi Septemba 2019.
MTAKA ametoa agizo hilo baada ya kuukagua mradi huo unaoanzia katika kijiji cha KARAGO hadi LAMADI wilayani BUSEGA na hadi kukamilika kwake unatarajiwa kunufaisha zaidi ya kaya elfu tano za kata ya Lamadi.
“Matarajio ya Serikali utekelezaji wa Mradi huu umalizike kabla ya Septemba 2019 ili uweze kukidhi mahitaji ya watu wa Lamadi na utumike vizuri na viongozi wa CCM watakaoomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi katika Serikali za Mitaa mwakani kundi utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo” alisema Mtaka.
Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt Raphael Chegeni pamoja na wananchi wa Lamadi wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza ahadi ya kuwapelekea maji wa mradi wa maji ambao utawasaidia kupata huduma ya maji safi na salama iliyo ya uhakika.
Mradi huo unaotekelezwa kwa miezi 24 unatarajiwa kugharimu jumla ya shilingi Bilioni TISA.
Katika hatua nyingine akiwa katika Mkutano wa Hadhara katika kijiji cha LAMADI Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametangaza kuwa biashara zifanyike kwa saa 24 katika Eneo (centre) la Lamadi Wilayani Busega.
“Eneo la Barabara Kuu ya Musoma Mwanza kutoka Benki ya Azania Tawi la Lamadi mpaka eneo la mwisho pale kwenye daraja letu, hili litakuwa eneo mahususi la kufanya biashara saa 24” alisisitiza Mtaka.
Amewataka wakazi wa Lamadi kuitumia kwa faida barabara Kuu ya Musoma-Mwanza na kituo(centre) kikubwa kinachoyakutanisha magari yaendayo mikoani na nchi jirani kwa kufanya biashara saa kama ilivyo kwa maeneo kama hayo katika mikoa mingine.
KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII BOFYA HAPA:http://simiyuregion.blogspot.com/2018/01/rc-mtaka-amtaka-mkandarasi-kukamilisha.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa