Simiyu Regional Commissioner, Hon. Anthony Mtaka has met with Chinese Ambassador to Tanzania Hon. Wang Ke.
Balozi Wang amefurahishwa na utekelezaji wa Mpango wa Simiyu wa One Product One Distict-(Wilaya Moja Bidhaa Moja) Maana China kwa sasa wanatekeleza One Belt One Road.
Aidha, ametoa vyerehani 50 kwa Mabinti wa Simiyu ikiwa ni kuunga Mkono juhudi za viwanda vidogovidogo mkoani Simiyu.
Balozi huyo pia amekubali kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kujenga bweni moja la watoto wa kike na amesema yupo tayari kusaidia ujenzi wa Maktaba ndani ya mkoa
Wakati huo huo amesema atasaidia kompyuta kuunga mkono juhudi za Mkoa kwenye Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(ICT) na kusaidia mkoa kupata jimbo rafiki nchini china pamoja na baadhi ya maafisa wa Simiyu kwenda China kupata uzoefu.
Vilevile ameuchagua Mkoa wa Simiyu kuwa mkoa wake wa Kipaumbele katika maeneo mengi ya miradi ya Kilimo,mifugo na uvuvi.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa