Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesaini Mkataba wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Msimamizi Mkuu wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa, Kapteni Fabian Buberwa.
Mkataba huo umesainiwa Aprili 30, 2019 mbele ya Wataalam wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na SUMA JKT katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini ambaye aliwataka SUMA JKT kujenga jengo hilo kwa viwango na kuhakikisha linakamilika kwa wakati.
“SUMA JKT mmepewa heshima kubwa na Serikai yetu na viongozi wetu pia tunaomba muendelee kufanya vizuri ili kulinda heshima yenu; tunaomba mfanye kazi usiku na mchana jengo hili likamilike mapema na ka viwango” alisema Sagini.
Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa, Kapteni Fabian Buberwa amemhakikishia Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini kuwa wakipata fedha watahakikisha wanakamilisha jengo hilo kwa wakati na kwa viwango vya juu, ili kuendellea kulinda heshima waliyopewa na Serikali
Naye Mhandisi wa Ujenzi wa Mkoa wa Simiyu, mashaka Luhamaba amesema Jengo hilo litakalojengwa eneo la Nyaumata Mjini Bariadi, litagharimu zaidi ya shilingi bilioni 5, 718, 387,926.20
Jengo hili linatarajiwa kuanza kujengwa mwezi Mei, 2019 na kukamilika baada ya miezi 18.
MWISHO.
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/05/ras-simiyu-asaini-mkataba-na-suma-jkt.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa