Ninafahamu kuwa leo tarehe 06/09/2017 vijana wetu walioanza darasa la Saba wanaanza mitihani yao ya siku 2 ikiwa ni hatua muhimu ya kuhitimu Elimu ya msingi.
Najua kwamba walimu, wazazi, walezi na viongozi wa ngazi zote wametimiza wajibu wao na wanafunzi pia wamejiandaa vizuri. Nachukua nafasi hii kuwaombea ufanisi vijana wetu wote wanaofanya mitihani kesho na keshokutwa.
Nawatakia heri watoto wote wa Mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla. Nawaombea utulivu wa akili na umahiri katika kujibu maswali yote ili wapate ufaulu ulio bora na hivyo kuanza vema safari yao ya kitaaluma.
Aidha, wasimamizi wote wafanye kazi hiyo kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kuwa na matokeo yanayoaminika. Baraka za Mungu ziwe kwenu nyote.
Jumanne Abdallah Sagini
Katibu Tawala Mkoa Simiyu
06/09/2017
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa