• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Rais Magufuli Aahidi Bilioni Nne Kuendeleza Ujenzi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Simiyu

Posted on: September 8th, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema atatoa kiasi cha shilingi bilioni nne  kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa hospitali ya Mkoa wa Simiyu na kuutaka Wakala wa Majengo hapa nchini (TBA) kujenga majengo hayo usiku na mchana, ili kuhakikisha yanakamilika katika kipindi cha meizi sita kama ilivyoahidiwa na Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.

Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo Septemba 08, 2018  katika Uzinduzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje la Hospiali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika mtaa wa Nyaumata mjini Bariadi, wakati akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.

Dkt Magufuli amesema kuwa atatoa shilingi bilioni nne ambazo zitasaidia kujenga majengo mengine ili wananchi wa Mkoa wa Simiyu na maeneo jirani waweze kupata huduma za rufaa huku akieleza kuwa  kutokana na umuhimu wa sekta ya afya shirika la Global fund wametoa shilingi bilioni 1.5.

“Leo ninafungua jengo hili na nakugiza Mhe. Waziri wasaidizi wako na TBA anzeni kupima majengo mengine yote yaliyobaki muanze leo fedha zitatatolewa, zipo za global fund bilioni1.5 zipo za Serikali bilioni 1.5 na mimi nawaongezea nyingine bilioni nne ziwe bilioni saba, ninachowaomba TBA mjenge usiku na mchana”  alisema.

 

Awali akitoa taarifa ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi Waziri wa Afya,jinsia ,wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa jengo hilo lianza kujengwa Novemba 2015 na kukamilika Mei 2018, limegharimu kiasi cha bilioni 2.1 ikiwemo na fidia ya eneo.

Ameongeza kuwa Wizra ya Afya itahakikisha miundombinu yote muhimu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa inakamilika, ili Hospitali hiyo iweze kutoa huduma bora kwa wananchi, ambapo amebainisha kuwa hospitali hiyo itapunguza mlundikano wa wagonjwa katika Hospitali Teule ya Mkoa ambayo ina hadhi ya Hospitali ya Wilaya.

Aidha, Mhe. Waziri Ummy  amemuahidi Mhe. Rais kuwa yeye kwa kushirikiana na wasaidizi wake watahakikisha majengo ambayo yatajengwa kwa kutumia fedha aliyoahidi kuitoa yanakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita, ambapo alisema kwa sasa huduma za wagonjwa wa nje, huduma za dharura, usatwi wa jamii na huduma za maabara vipimo vya kawaida zinatolewa  

  

Ummy pia alibainisha kuwa katika bajeti ya mwaka 2018/2019, Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Mkoa ambayo kukamilika kwake kutawapunguzia wananchi wa Simiyu kufuata huduma za rufaa katika Hospitali ya Rufaa ya  Bugando jijini Mwanza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema katika mwaka wa fedha 2017.2018 mkoa wa Simiyu umepokea shilingi bilioni 11 kwenye sekta ya Afya ambapo Vituo vya Afya 39 vimejengwa na kukarabatiwa pamoja na bilioni mbili kwa ajili ya ununuzi wa dawa.

Pamoja na kufungua Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Mhe. Rais Magufuli amefungua Mtandao wa barabara za lami Mjini Bariadi zilizojengwa chini ya mradi wa ULGSP, kuweka jiwe la msingi mradi wa maji Lamadi na kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Bariadi-Maswa inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 49.7.

Sepemba 09, 2018 Mhe. Rais Magufuli anaendelea na ziara mkoani Simiyu ambapo atapita na kufanya mkutano wa hadhara Lagangabilili Itilima na kuelekea Meatu.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:https://simiyuregion.blogspot.com/2018/09/rais-magufuli-aahidi-bilioni-nne.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa