• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Rais Magufuli Aagiza Wizara ya Ujenzi, TANROADS Kusimamia Ujenzi Daraja la Sibiti na Kutaka Likamilike Machi 2019

Posted on: September 10th, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi. Isack Kamwelwe na Mtendaji Mkuu wa TANROADS kusimamia Ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti linalounganisha mikoa ya Simiyu na Singida na kuhakikisha linakamilika ifikapo Machi, 2019.

Rais Magufuli ameyasema hayo Septemba 10, wakati akizungumza na wananchi wa mikoa ya Simiyu na Singida katika Kijiji cha Nyahaa wilayani Mkalama Mkoani Singida muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja hilo.

Amesema daraja hilo limeanza kujengwa muda mrefu na akazikataa sababu zilizotolewa na Mkandarasi kuwa zimepelekea kuchelewesha ukamilishaji ikiwemo mkandarasi kufanya kazi miezi minne tu kwa mwaka kutokana na eneo hilo kuwa na maji mengi hususani kipindi cha mvua.

"Wananchi wa hapa wanahitaji daraja limalizike hawahitaji sababu, mkandarasi alipokuwa akiomba kazi hakujua kuwa hapa maji huwa yanapita, ma-engineer hawakujua? Hapa hakuna sababu,msitafute kisingizio"

"Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote, Mtendaji Mkuu TANROADS nataka daraja hili sasa likamilike, mimekuja kwa makusudi kuweka jiwe la msingi nataka siku nikirudi nipite juu" alisema Rais Magufuli

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi. Isack Kamwelwe amesema Daraja la Mto Sibiti likikamilika litakuwa mkombozi katika kuunganisha mikoa ya Kanda ya Ziwa na mkoa wa Singida na kuahidi ujenzi wa kilomita 25 za lami kwenye tuta la daraja hilo.

"Daraja hili limejengwa katika viwango vya juu sana, tuta lake pia limejengwa kwa kiwango cha juu sana na tayari tumeshaongea na TANROADS kwamba kupitia kwenye fedha za matengenezo, tuta hili kwa karibu kilomita 25 tutaziweka lami Mhe. Rais, tutaposhindwa tutakupa taarifa"

Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi. Patrick Mfugale amesema kazi ya Ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti inayofanywa na Mkandarasi Hainan International Limited kutoka nchini China na mpaka sasa umefikia asilimia 70 na hadi kukamilika kwake litagharimu jumla ya shilingi bilioni 16.3.

Rais amehitimisha Ziara yake ya siku tatu mkoani Simiyu Septemba 10, ambapo akiwa Simiyu alipata nafasi ya kuweka mawe ya msingi, kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali kupitia mikutano ya hadhara.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:https://simiyuregion.blogspot.com/2018/09/rais-magufuli-aagiza-wizara-ya-ujenzi_11.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa